FFU wa Ngoma Africa kuvamia AFRO-Ruhr Festival !Mjini Dortmund, UJerumani jumamosi 30 Juni 2012

Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU yenye makao yake kule Ujerumani,wanategemewa kukwea jukwaa la Afro-Ruhr Festival, siku ya jumamosi 30 Juni 2012 mjini Dortmund,Ujerumani.

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya inayoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja wa FFU,itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika onyesho hilo kubwa la aina yake,washabiki wa muziki katika onyesho hilo wanakumbana "Jino kwa Jino" na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band aka FFU, bendi hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za "Supu ya Mawe" ,"Uhuru wa Habari" na "Bongo Tambarare" ambazo ipo katika CD ya "BONGO TAMBARARE" pia zinasikika katika kambi yao FFU at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2012

    Kile kikamanda ketu Ras Makunja,kimeanza tena?
    na mabaraha yake

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2012

    Kile kikamanda ketu Ras Makunja,kimeanza tena?
    na mabaraha yake

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2012

    Kamanda mkuu wa ffu,chonde chonde baba...na makombora ya machozi,uwe na huruma kamanda

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2012

    Sio mchezo vichaa ffu wanafanya kweli,na kazi yao tunaikubali

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2012

    Kaka kamanda ras makunja na kikosi shughuli ngoma afrika aka ffu aka watoto wa.....mbw? kazi zenu nzuri,lakini kufanya kazi na mkuu wa kikosi inakua ngumu..masharti ya msanii kugeuka mjeshi ni hatari hakuna enjoyment

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2012

    kamanda mkuu ras makunja mie nipo bongo naomba kazi,lakini uwanajeshi siuwezi wa kuperekana mbio kila kona

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2012

    ffu onyesho lenu la 2010 Hamburg,mnakumbuka washabiki wenu walivyosongamana na kusababisha mtu kupoteza maisha? ndio maana mwaka jana 2011 promoter wenu alipewa masharti magumu na manjago wa hamburg,kama anawataka lazima ulinzi uwe mkubwa kwa gharama zake,bahati yenu nasikia mwaka huu umekubaliwa tena.chungeni sana uha ni zawadi kila kiumbe kutoka kwa mola wetu.
    Mdau
    Hamburg

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 23, 2012

    naona kama Ras makunja umeimarisha ulinzi siku unapiga doria na chui badala dog domobaya

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 23, 2012

    naona kama Ras makunja umeimarisha ulinzi siku unapiga doria na chui badala dog domobaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...