Mbunge wa Korogwe Vijijini(CCM) Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu", akizungumza na waandishi habari
-
Mbunge wa Korogwe Vijijini(CCM), Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu", akizungumza na waandishi habari mjini Dodoma jana, amekanusha madai kuwa alilieleza Bunge kuwa mkasa uliompata Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari na Kamati ya kufuatilia haki zao, Dkt. Steven Ulimboka, kuwa alistahili, SI YA KWELI na KUOMBA RADHI Madaktari nchini kwa jinsi alivyonukuliwa vibaya wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni tarehe 28 Juni 2012.

Jana, Mbunge huyo alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa alisema, "kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata wagonjwa wengine mahospitalini."

Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni, ambapo  Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda  alilazimika kuingilia kati kumzuia Ngonyani asiendelee kutoa kauli hiyo kwa vila suala la madaktari bado liko Mahakamani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2012

    Awe kasema au hakusema, nadhani waliyoyasikia hayo maelezo yake ndio wataweza kubaini au ku-judge ukweli uko wapi, kama alistahili au hakustahili to speak his mind. Freedom of speech jamani, tatizo letu hatujiamini na kuwa wa wazi to free our mind. tumekuwa woga woga tu huku tukisemea chini chini na yanapoonekana kukera na kudhihiri, ndio hapo inakuwa mshike mshike na kuanza kuombana radhi upya. Pole sana Dk. Ulimboka, uguwa pole na Mola takujaaliye upone salama.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2012

    Huyu jamaa ni wa ajabu sana. Hili la kukanusha alilolisema bungeni halishangazi. Kuna wakati mganga huyu wa kienyeji alidai kuwa picha iliyotoka gazetini ikimuonyesha akiwa na Vincent Nyerere na Joshua Nassari wa Chadema wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki imetengenezwa! Alitishia kwenda mahakamani lakini aliumbuka pale gazeti hilo lilipotoa picha zaidi zikimuonyesha akiwa na watu wa Chadema.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2012

    Huko bungeni hakuna waganga wa kienyeji tu, kuna masharobaro, ma DJ, ma sistaDO, WANA BONGOFLAEVA, NA SHOW MAN AND WOMEN. Wengine wanapigania haki za wacheza shoo waendelee kuonesha vya siri vyote kila kukicha. Na huwa wanasema ovyo kwelikweli wakati mwingine. Bado ile sheria ya Cameron ikikubalika tutaona na hao jamaa humo ndani wakipigania haki zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...