Habari Ankal Michuzi na Watanzania wote.
Naomba uniwekee katika Blogu yako Ushauri wangu kwa Idara ya Uhamiaji Tanzania na hasa kwa Zanzibar.

Passport za Zanzibar zimekuwa zikitolewa bila kufuata ujazaji wa fomu,kwa ushahidi wangu mwenyewe na wa mwenzangu.

Mfano .

1.Passport yangu ya Mwanzo imetolewa kwa Jina la MOH'D na kwa kuwa Ulaya wanafuata kilichoandikwa "Name as appeared in the Passport or Travel document" kwa hiyo jina linajulikana ni MOH'D,sasa cha kushangaza ni kwamba nilipoomba tena Passport kutokana na uchakavu wa Pasi ya Zamani jina limeandikwa Mohamed kwa kirefu.

sasa imepelekea kutokubaliwa kwa maombi ya ukaazi hadi wapate uthibitisho kuwa MOH'D ndio ile ile Mohamed process ambayo imechukua muda mrefu kutokana na kwamba hatuna Balozi wala Consulate wa Tanzania au hata wa Africa anotuwakilisha.

Licha ya kuwa kuna Muhuri ndani ya Pasi kuwa passport ya zamani imekuwa Withdrawal/cancel/lost lakini nimeambiwa bado haitoshi kutokana na kilichobadilika ni Jina, ilitakiwa barua ya mahakamani kuthibitisha hilo na form nilijaza kama Pasi ya zamani inavoonesha MOH'D.
Pili.Ushauri kwa VYETI VYA KUZALIWA NA VYA NDOA AU KARATASI ZA FAMILY STATUS NA NYENGINEZO zinazotoka Zanzibar,(sikusudii kuchafua mambo ya Muungano ila kuturahisishia tu kwa sasa) tungelipenda ziandikwe The United Republic of Tanzania,BADALA ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,hili ni tatizo kutokana Zanzibar haitambuliki na haimo kwenye Database zao sasa inatupa shida sana tunatakiwa tutengeneze vyeti vya TANZANIA na kwa Zanzibar sijui vinatoka wapi,wala Dar es Salaam sijui wapi vinatoka kwa hiyo ni bora mfumo uwe mmoja tu au angalau liandikwe neno United Republic.

Ni hayo tu kwa kuwa hadi sasa hakijaeleweka inabidi nianze process mpya kufuatilia karatasi zote Tanzania hadi kupigishwa mihuri ubalozi na commonwealth pia translation na kufunga safari kwenda U.K kufuatilia.

Ahsante.
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2012

    Yalikwishanikuta pia kwenye passport yangu. Ya zamani iliandikwa Samuel na documents zangu zote za shule na uhamiaji huku ughaibuni zinakwenda kwa jina hilo. Baada ya kuomba pasi mpya za elektroniki,wakanipa jina la Samwel. Ninachoshukuru ni kwamba sijapata tatizo so far!
    Kwa hiyo inaonekana ni tatizo sugu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2012

    This is Serious mistake. ila Bw Mkubwa unapopewa nyaraka unatakiwa uthibitishe kuwa ni sahihi. Kwa mfano hiyo MOH'D ulitakiwa uikatae mapema sana.
    Pili nakubaliana na wewe kuwa nyaraka zote za kutumika kimataifa mf. vyeti vya ndoa kuzaliwa nk. nenda hapo Dar es salaam, RITA wape vyetui vyako vya ndoa au kuzaliwa watakupatia nyaraka za kutumika kimataifa. Hawana shida kabisa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2012

    mdau pole sana sana,maana kufuatilia mambo ya uhamiaji tu hapa UK ni kazi kubwa halafu ukaweke ya Zanzibar kweli utapa ukaaji kweli?nakutakia kila la heri maana unakazi.mdau Walthamstow.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2012

    vyeti vya ndoa na kuzaliwa kwa bara (dar) vinapatikana ktk ofisi za wakuu wa wilaya kama utaratibu utakuwa haujabadilika na naamini haujabadilika.(mimi niko zanz kwa mda mrefu sasa).lakin ukifika hapo (kwa ofisi za mkuu wa wilaya) watakupa maelezo endapo kama utaratibu utakuwa umebadilika lakin naamini haujabadilika.

    pole kwa yote.

    kama vipi nipo hapa loptz@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2012

    MOH'D ndio nini? na linatamkikaje? acha kuharibu jina la mtume muhammad Moh'd kwa ki english ni: the dog with big mouth. Rekebisha jina lako acha kutuaabisha na malalamishi yako yasiyozingatia uhalisia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2012

    Hakuna kitu kama hicho znz ni nchi na inapaswa kutoa passport zao kama nchi kwahiyo ya znz yache znz wewe fuatiilia unapoona unaweza kupata pasi yako kama ww ni mtu wa bara fuatilia dar mpaka upate huo ushauri wako hautakubalika hata mm siikubali.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2012

    Mdau kaongelea la Kweli hapa Hii tabia sio Zanzibar tu Hata huku Bara na mwisho unajikuta una passport mbili.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 21, 2012

    Kuhusu 'Mohammed/Mohamed' kuandikwa 'Moh'd'ni kosa kubwa sana na ni lazima lirekebishwe.
    Ama kuhusiana na Vyeti vya kuzaliwa, vya ndoa au karatasi za family status na nyinginezo hapo sikubaliani kabisa kubadilishwa kutoka hali yake ya leo na kutambulishwa kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!!! As long as we Zanzibaris are in the process of being re-liberated I strongly oppose your nonsense suggestion.

    ReplyDelete
  9. ushauri: ukipewa document YOYOTE hakikisha haijakosewa au imeandikwa vile wewe unavotaka.
    kuhusu swala la ndoa na mambo mengine (yanayofanana na hayo)..Znz na Bara zinakuwa regarded as mamlaka mbili tofauti na kuna sheria tofauti, ila ukitaka zitambuliwe nje utapaswa kuzipeleka Wizara/Idara ya Mambo ya Nje ili zithibitishwe

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 21, 2012

    Alichokisema mdau ni sahihi. Haya yanatokea hata katika vyeti vya kumalizia shule na kwengineko. kwamfano, Othman ataandikwa Athumani. Salim ataandikwa Salmini, Juma ataandikwa Jumaa.Ambapo ni kinyume na muhusika alivyosajili jina lake.

    Kama mdau kaamua kuandika jina kwa ufupi tokea mwanzo hiyo ni hiyari yake kwani anaejua ni yeye na simwengine. wapo hata wanaoandika MD ikimaanisha Mohammed. katika nchi za Asia ya kusini nikawaida watu kutumia MD ikimaanisha Sawa na Mohammed.

    Kuhusu vyeti vya kuzaliwa katika kipindi cha miaka ya sitini mpaka sabiini nembo ya serikali ya Muungano ikitumika kuonyesha cheti ni mali ya Tanzania.

    lakini, yalikuja mabadiliko miaka ya themanini baada ya Zanzibar kupitisha rasmi matumizi ya nembo yake ya SMZ kutumiwa katika nyaraka zake. Kwahivyo shughuli hizo si za muungano ama kwa mawazo yako ni kuengeza kero za muungano.



    Tuwajibike ipasavyo inawezekana.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2012

    did you say nonsense ?? angalieni huyu naye ,yale yale .Mwenzio kasema jambo safi na la maana wewe umekuja na mkojo wako wa kumona hafai na eti punguani, na ukweli ni kwamba hata huko zanzibar ulishakimbia zamani ila basi tu unatuharibia nchi. zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 21, 2012

    Wadau tujaribu kumuelewa huyu mto mada. Jina lake ni MOH'D na siyo Muhammad. Tukianza kuangalia maana ya majina, sidhani kama ni sawa. Mimi prifesor wangu anaitwa Suzuki Kumamotto. Haikunichukua muda kuelewa kuwa lazima tuheshimu na kuyatamka vizuri majina ya watu bila kujali yana maana gani.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 22, 2012

    hiyo haipo zanzibar tu, huku bara dada yangu kapewa passport kwenye jinsia wameweka male wakati ni mwanamke.Na form alijaza female yaani we acha tu.

    ReplyDelete
  14. Nyie wazanzibar mkiwa huku ulaya huwa mnaukataaga Utanzania badala yake mnasema nyie ni wazanzibar na sio watanzania mpaka mnapopata matatizo kama haya ndio mnakuja kuukumbatia utanzania...haya sasa tuone huo uzanzubar wenu kama utatatua taizo ilo

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 22, 2012

    Hii ni kweli kabisa,si kwa Muhamed tu bali majina mengi,khamis,hamis,huseni hussein,yote matatizo yananzia kwenye veti vya kuzaliwa na pia ni uvivu wa wahusika,Utaandikaje jina Moh'd kwenye pasi ya mtu? wenzetu kubadilisha jina hadi mahakamani kama sikosei na hupatiwi kitu kabisa kama hakuna kuthibitisha.

    Kuhusu vyeti vya ndoa na si vya Kuzaliwa kuandikwa serikali ya Zanzibar ni kweli kabisa kwanza veti vya Zanzibar ukipeleka Italy ubalozi wa Tanzania wanaanza kukukatalia kabla hata havijafika vilipokusudiwa utaambiwa Feki-na kuhusu Kuhakikisha ukizingatia huna balozi na umetumiwa na labda DHL utakataa wapi na kitu kishafika KUMBUKENI nchi nyingi maswala ya Kujiandikisha inakuwa muda maalum na ukipitiliza there is no Excuse mfano Hapa Umangani-na juzi juzi kule Poland.

    pOLE MDAU HAYO YAMEWAKUTA WENGI SANA

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 22, 2012

    Zanzibar wanataka nchi yao juzi nilimuuliza mganga mmoja wa kienyeji pale mnazi mmoja na baada ya kupiga ramli zake kwa karibu nusu saa akaniambia kuwa nchi yao wazinzibari wataipata sio muda mrefu kuanzia sasa.

    Sasa kwa kauli ya mzee huyu amabe namuamini sana inabidi hao walioko uhamiaji huko zenj wajikaze kwani wakisha pata nchi yao makosa kama haya inaweza yakawafanya waonekane wamelilia nchi huku uwezo wa kuandika majina yao sawa sawa unawashinda sijui huko kuongoza tena ndio itakuwa chenga twawala.

    haya tukaneni mlango uwazi mliokasieika mimi nina mood nzuri leo nimeamua kukuchokozeni nifurahi nafsi.

    mdau.

    India.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 22, 2012

    Zanzibar hakuna pasipoti. Pasipoti zinatolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama inavyoonyesha kwenye kopi ya pasi yako!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 22, 2012

    Kwani Zanzibar ni nchi?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 22, 2012

    Mdau wa 6 hapo juu Anonymous wa Thu Jun 21, 06:43:00 PM 2012
    -----------------------------------
    .....Hakuna kitu kama hicho znz ni nchi na inapaswa kutoa passport zao kama nchi kwahiyo ya znz yache znz wewe fuatiilia unapoona unaweza kupata pasi yako kama ww ni mtu wa bara fuatilia dar mpaka upate huo ushauri wako hautakubalika hata mm siikubali....
    -----------------------------------
    MMEONA SASA?

    DUNIA NZIMA HADI KWA HAO WALIOWAHI KUTUTAWALA HAWAITAMBUI ZANZIBAR KAMA NCHI INAYOJITEGEMEA!!!

    NINA UHAKIKA KABISA HATA HIYO OMANI YENU KATIKA DATA BASE ZAKE HAINA ZANZIBAR NCHI INA ZANZIBAR KAMA SEHEMHU YA 'THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA' KAMA MNAVYOONA UBALOZI ULIOPO OMAN NI WA MUUNGANO SIO 'JAMHURI YA ANZIBAR' PAMOJA NA WAO OMAN KUWAHI KUWATAWALA ZAMANI.

    MUWE MNABISHANA KWA AKILI ZAIDI,

    HIVYO MNAPODAI MUUNGANO KUVUNJIKA MNAPOTEZA MUDA BURE, ANGALIENI HADI KATIKA DATA BASE SYSTEMS ZAO HAKUNA JINA LA NCHI YA ZANZIBAR !

    MPO HAPO???

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 22, 2012

    Zanzibar nchi?

    Mtachemsha mawe !!!

    Kama ni hivyo mkipewa ninyi Zanzibar tutegemee hata Ukerewe (Kisiwa ktk Ziwa Victoia ) nayo itadai Uhuru kama ninyi Zanzibar itataka nayo ipewe nchi!

    Ina maana kila Wilaya na Mkoa katika JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA itadai ipewe Uhuru wake!

    Hata huko UN hawaitambui Zanzibar kama nchi kamili, sasa mnaotaka kuvunja Muungano Jumuia ya Kimataifa itawachukulia kama ni WAASI WA SERIKALI HALALI ILIYOKO MADARAKANI NI VILE HAMTAPATA USHIRIKIANO WOWOTE MADAI YENU YATAPOKELEWA YATAFIKIRIWA LAKINI NI WAZI YATAPUUZWA.

    NA HATA KAMA MKITUMA MAOMBI UMOJA WA MATAIFA YATATUPILIWA MBALI !!!

    FANYENI AKILI MKALIME LABDA MTAVUNA MAZAO AMA MKAVUE SAMAKI BADALA YA KUPOTEZA MUDA KUPINGA MUUNGANO HALALI !!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 22, 2012

    Zanzibar mafuta mafuta!

    Ahhh ombi la kuvunja Muungano rasmi mimi mwananchi wa kawaida ninalikataa kata kata, kwa kuwa tumeshashibana,,,watu wamekuwa wakioana Bara na Visiwani!

    Mimi binafsi kama Mwanaume wa Bara siwezi kukubali kuachia Wanawake wa Visiwani ambao wana mafuta mafuta ya Uarabu kwa kweli wanawake wa Visiwani ni 'watamu' hata kwa macho!!!,,,Mashallah.

    Hili wazo la kuvunja Muungano hapana kabisa, ni 'Ibara' isiyotekelezeka,,,tusirushiane ndege wetu wenyewe kwa wenyewe!

    Nafasi pekee ya sisi Wabara kupata wanawake wa Kiarabu ni kupitia Zanzibari tu,

    Sasa sisi akina Maganga wa Bara tutaponea wapi?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 22, 2012

    Wanawake wa Visiwani watamu:

    Unguja na Pemba ndio kwenye marashi ya karafuu,

    Sasa mnatulete ujinga wa eti pyeee, tunataka kuvunja Muungano !

    Sasa kwa mwanaume kamili hawezi kukubali kuachia kitu 'kitamu' suala hilo haliwezekani, TUACHE MJADALA WA KUUVUNJA MUUNGANO TUJADILI MASUALA KAMA HILI LA MAREKEBISHO YA PASIPOTI !!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 22, 2012

    Hitilafu ndogo ya Pasipoti ya Mwananchi aliyepo nje ya nchi haiwezi kusababisha tuvunje Muungano!

    Mfano ni jambo gumu kuamriwa na wachonganishi kumpa Talaka Mkeo uliyempenda na kuzaa naye watoto huku mkiwa na maelewano mazuri!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 22, 2012

    Tujadili suala la marekebisho ya Pasipoti ya mwenzetu aliyeko huko Majuu halafu aelekezwe Ofisi ya Uhamiaji akapewe Pasi sahihi,,,

    Hizo nchi kubwa Marekani,UK, na Zingine huwa zinakosea ktk nyaraka nyeti kama Pasi,Vyeti vya Usajili,Vyeti vya Kuzaliwa na vinginevyo itakuwa Tanzania?

    Lakini 'ujinga' kama kuvunja Muungano msiulete hapa ktk Makala hii.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 22, 2012

    Tujadili Pasipoti lakini ni Wanawake wa Visiwani ni 'watamu' kwa mengi likiwemo ile kuzungumza tu sauti, mapozi yao na Kiswahili chao mtu mwanaume anakuwa ameridhika kabisa!

    Sasa mnaleta ujinga gani tena?,,, Muungano uvinjike halafu nimfuate mke wangu Zanzibar kwa kuomba visa tena?,,,au mke wangu wa Visiwani aishi na mimi mumewe Bara kwa Kibali cha Uhamiaji?

    Mashallah,,,na Udumu Muungano wa Bara na Visiwani!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 22, 2012

    Pasipoti ya mtu nje ya nchi inamakosa, halafu eti tuvunje Muungano huku wakati nina mwanamke wa Kizanzibar namiliki!

    Khaa, mnaleta ujinga gani tena ?

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 22, 2012

    mchangiaji wa mwisho katoa bonge la pointi!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 23, 2012

    KUNA MCHANGIAJI MMOJA ANASEMA ETI ZANZIBAR WAKIDAI NA UKEREWE NAO WATADAI,HUYU MWEHU AU MZIMA LAKINI KWANI TANGANYIKA ILIPOTAKA USHIKAJI NA ZANZIBAR NA KUUNGANA 1964 UKEREWE ILIKUWA SEHEMU YA UGANDA? BAADAE NA WAO UKEREWE WAKATAFUTA USHIKAJI NA TANGANYIKA?

    UKEREWE NI SEHEMU YA TANGAYIKA NA ZANZIBAR ILIKUWA HAINA UHUSIANO WOWOTE NA TANGANYIKA NDIO MAANA MKAOMBA TUUNGANE SASA TUMESHTUKA HATUTAKI MNAANZA KULETA HABARI ZA UKEREWE NA MIKOA YENU SISI HAITUHUSU KITU HIYO DODOMA NA TABORA HUKO KWENU SIO KWETU NA ZANZIBAR ILIKUWA NA KITU UMOJA WA MATAIFA BAADA YA MUUNGANO NDIO KIKAONDOLEWA NA KUTUMIKA KITI CHA TANGANYIKA NA KUBATIZWA JINA LA TANZANIA SASA UKEREWE AU KIGOMA YAKO WALIWAHI KUWA NA KITI KATIKA UMOJA WA MATAIFA?

    USIONGEE PUMBA NCHI ILIYOWAHI KUWA NA KITI KUKIRUDISHA SIO KAZI NCHI KADHAA ZIMERUDISHA VITI VYAO NA KUWA NCHI KAMILI SISI TUNAVUNJA MUUNGANO MKITAKA MSITAKE TENA KAZI KWENU KAMA MIKOA MLIYO NAYO HAIWATOSHI NENDENI MKAUNGANE NA ZAMBIA SI MNA RELI MOJA NAO AU UGANDA UNGANENI NAO MNAOGOPA NINI IDDI AMIN KESHA KUFA.

    ASANTENI.
    MDAU

    ZENJ.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 23, 2012

    MDAU WA HAPO JUU ANONYMOUS WA Sat Jun 23, 01:49:00 AM 2012

    MUUNGANO HAUVUNJIKI NG'O !

    UTAKUFA WEWE MUUNGANO UTAUACHA

    TATIZO KUBWA NI KUWA HATA MKIPIGA KURA VISIWANI MNAOTAKA MUUNGANO UVUNJIKE MTAZIDIWA NA WASIOTAKA UVUNJIKE.

    PANA AINA 2 YA WAZANZIBARI:

    1.WAZANZIBARI WENYE NJAA NA WALIOKWAMA KIMAISHA , NI WALE AMBAO WENGI WAPO NJE YA NCHI NI WAKIMBIZI HUKO MAJUU NA WENGINE WAPO HUKO HUKO VISIWANI HALAFU HAWANA MIPANGO. (HAWA NI KAMA CHINI YA 25% YA WAZANZIBARI WOTE AKIWEPO WEWE ANONYMOUS WA Sat Jun 23, 01:49:00 AM 2012

    2.WAZANZIBARI WANAOISHI BARA NA WENYE MAFANIKIO YA KIFEDHA NA MAISHA WAHA NI ZAIDI YA 75%

    HIVYO KUNDI LA KWANZA 25% WAPINGA MUUNGANO LINA WIVU NA CHUKI DHIDI YA KUNDI LA WAZANZIBARI 75% WANAOUNGA MKONO MUUNGANO NA WENYE MAISHA YAO

    SASA MADAI YAKO NA WENZAKO HAYATATIMIA (mkipiga Kura za maoni mtashindwa) HATA JUA LIKIWAKA USIKU NA KUZAMA MASHARIKI BADALA YA MAGHARIBI !!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 23, 2012

    Anonymous wa Sat Jun 23, 01:49:00 AM 2012

    WEWE MDAU WA ZENJ,

    Mdau wa 28 hapo juu hebu angalia kwanza HUYO ALIYEKUWA NA TATIZO LA KUKOSEWA JINA KATIKA PASIPOTI YAKE HUKO MAJUU NI MZANZIBARI MWENZIO.

    TAZAMA MANENO YAKE AMEGUNDUA KUWA NI LAZIMA AUTAMBUE MUUNGANO KWA KUWA ZANZIBAR HATA KATIKA DATA BASE ZA MATAIFA YOTE DUNIANI HAITAMBULIKI KAMA NCHI.

    YEYE MTAZAMO WAKE NI WA MTU MWENYE AKILI NZURI KULIKO WEWE NA WENZIO WAPINGA MUUNGANO BILA AKILI.

    MNAPOPINGA MUUNGANO MUWE NA MITAZAMO YENYE AKILI LAKINI ZAIDI YA HAPO MTAPOTEZA MUDA WENU BURE !!!,,,NI AFADHALI MNGECHUKUA NYAVU MKAVUE SAMAKI BWEJUU MNGEFAIDIKA LAKINI SIO KUPINGA MUUNGANO BILA KUWA NA AKILI TIMAMU.

    HUYO JAMAA ALIYEPO MAJUU ULAYA NI KATI YA WATU MUHIMU WANAOFAA KWA KUWA ANAJUA FIKA KUWA AKIUPINGA MUUNGANO ATAKUWA AMEKALIA KUTI KAVU KWA KUWA YEYE SIO ''CITIZEN OF ZANZIBAR'' (Kwa kuwa Zanzibar sio nchi hata hayo Mataifa yanathibitisha kwa kutokuwa na data base hiyo) BALI NI KUWA YEYE ANATAMBULIKA KAMA RAIA WA ''THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA''

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...