Wakati tunapoelekea katika shamra shamra ya sikuu ya Saba Saba,
watanzania tunafurahia sikuu hii kwa kupata burudani ya raha ya nyimbo
mpya zilizopo katika CD "Bongo Tambarare" kutoka kwa bendi maarufu ya
muziki wa dansi Ngoma Africa Band aka FFU yenye maskani nchini Ujerumani, CD hiyo yenye nyimbo tatu "Bongo Tambarare" , "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari" imeshaanza kupiga hodi katika milango ya vituo mbali mbali vya redio duniani na hapa nyumbani itasikika wakati wowote kuanzia sasa ili watanzania wenye Bongo Tambarare yawe wapate raha ya muziki.
CD hiyo yenye nyimbo tatu zilizojaa ujumbe wenye furaha na mafunzo kwa jamii, kama vile "Supu ya Mawe" ni utunzi na wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU akiimba kwa kushirikiana na mpiga solo afande Chris-B. Watanzania tuipokee CD "Bongo Tambarare" na tufurahie Saba Saba kwa kupata raha ya "Supu ya Mawe" kutoka kwa Kikosi kazi Ngoma Africa aka FFU.
unaweza kusikiliza pia at www.ngoma-africa.com




Enhhhh bngpo Tambarale na Supu ya Mawe.
ReplyDeleteSupu hii ya mawe ndio ya kuzimulia baada ya kunywa gongo la mabibo!
kichwa cha habari kina makosa. Kiswahili sahili wanasema kupeleka, na siyo kupereka
ReplyDeleteFFU wana visa vya kila aina sasa hii supu ya mawe jamani tutakunywa vipi?
ReplyDeletesasa kwani akina ffu hawalali usingizi ? vichaa wetu ffu kila kukicha lazima wataibuka na mpya na kutingisha umma,au kuna nguvu za kiza nyuma yao?zinawaongoza.
ReplyDeleteEbwana eeeh,
ReplyDeleteWana wa Ras Makunjas inabidi mfanye mpango wa makaratasi kabisa huko Majuu kwa njia yeyote ile iwe hata ya Vibali vya Uganga wa Kienyeji maana Wazungu Taaluma hiyo hawana, ikishindikana Ndoa na Vikongwe!
Kwa vile mkijipindua tu kurudi Bongo kwa jinsi mlivyolizima na kukaa sana huko ni wasi Mjerumani hatawapeni tena visa!
Msirudi Bongo kihasara hasara msije mkabaki na ziara za Msumbiji na Malawi!
Jeremani ndio Mshirika mwenye roho ya ngumu kabisa, mashariti na sheria kali katika nchi zote za Umoja wa Ulaya.
Jeremani mchezo?
Sasa Ankal Michuzi hii supu ya mawe si hatari tupu maana inawekukwama kooni,hivi kichwani mwa huyu mtunzi mna kitu gani?
ReplyDeleteSasa Ankal Michuzi hii supu ya mawe si hatari tupu maana inawekukwama kooni,hivi kichwani mwa huyu mtunzi mna kitu gani?
ReplyDeleteKiswahili sanifu ni "Tambarale".
ReplyDeletewewe anony wa 01:04 2012,
ReplyDeleteSasa unawashauri akina ras makunja watafute makaratasi,una mawazo gani? unadhani kuwa miaka yote hiyo ndio wasiwe na makaratasi au vibali vya kuishi ujerumani. usiwe na mawazo kila mtu anayeishi ulaya ni mdandia meli au anaishi kiujanja ujanja
kamanda ras makunja wakati mwingine unaanzisha baraha na nyimbo zako,sasa supu ya mawe kamanda wetu tutainywa vipi? kama si kuwatafuta watu ubaya
ReplyDelete