Bendera za CCM zilizopambwa kwenye Uwanja wa Community Cetre, Mwanga, mkoani Kigoma, zikiwa zimeunakshi uwanja huo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa CCM utakaofanyika leo Jumapili.
Mafundi wakiandaa jukwaa kwa ajili ya mkutano huo, kwenye Uwanja wa Community Cetre, Mwanga mkoani Kigoma. mkutano huo ni leo Jumapili, Julai 22.
Mafundi wakiwa katika pilika pilika kuandaa jukwaa kwa ajili ya mkutano huo.
Wananchi wa mkoa wa Kigoma, wakiwa katika maandalizi ya mkutano wa CCm kwenye Uwanja wa Community Cetre, Mwanga leo.
Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma, iliyopo Mwanga.
Barabara ya Mwanga hadi Kidahwe mkoani Kigoma ni miongoni mwa maendeleo inayojivunia CCM katika utekelezwaji wa ilani yake.
Choo bora cha kisasa kilichojengwa kwenye mwalo wa Kibirizi wa kuengesha mitumbwi ya kusafirisha mizigo katika ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.
Hilo jukwaa lazma liende down wakipanda wahishimiwa na vitambi vyao.
ReplyDeleteyaani ujenzi wa choo ni jambo la kujivunia ktk utekelezaji wa ilani ya ccm? je, wana kigoma mko tayari kusubiri miaka mingine 48[toka tupate uhuru] ili mjengewe choo??
ReplyDeleteWhat about that road au hujaiona au ndio siasa za kitoto kupinga kila kitu..zitto kabwe mwenyewe anakili hakuna raisi aliyeiendeleza kigoma kama kikwete-ccm
Deletewewe ,mbao imara hizo au mpaka liwe la chuma ?? nyie watu daima kutuponda tu,sijui na wewe unatokea huko huko kwa kina M.United.Zebedayo
ReplyDeletehe !! wewe uliona wapi kwingine choo kina mbao za mwininga ?? Huko Ulaya mbao kama hizi zinajengewa counter za kina David Cameron, bwana heshimu mwininga ndugu yangu. nakumbuka kwamba ,tulikuwa tumetawaliwa kwa kipindi kirefu ,na mzungu katuibia mali nyingi na kapeleka kwao enzi hizooo !! siyo sasa hivi maana siku hizi tuna macho na tunayatumia , ndiyo maana unaona kina Vodacom wanachuma lakini nusu yake inabaki hapa hapa na tunaziona shughuli za pesa zao jinsi zinavyotusaidia kuleta maendeleo. ingelikuwa hivi tangia enzi ya mkoloni, basi vyoo kama hivi vingelikuwa kila mtaa. kwa hiyo ,kama mnavyosema huko, we are on the right track. Zebedayo
ReplyDeleteRetarded bunch of dushbugs
ReplyDeleteKigoma ilitelekezwa kama pwani tu na sababu zinajulikana. Karibu mashekhe wakubwaTZ wote wanatoka KG.
ReplyDeleteAnon. no. 6 nakubaliana nawe. Hata hivyo Kigoma ya miaka hiyo na wilaya zake sio ya leo hii, nimewahi kuishi pande za huko (Kibondo) arround 90's lakini nilipotembelea hivi karibuni, kwa kweli siyo ile Kibondo niliyoiacha wakati huo, kumekuwa na maendeleo na mabadiliko ya haraka na yenye matumaini, kuanzia barabara mpaka majenzi na hata maendeleo ya jamii kwa jumla, japokuwa hayajafikia standard inayotakiwa, lakini inatia moyo na matumaini kwa kiasi fulani. Tunaamini ipo siku na Kigoma pia yaweza kuwa ni miongoni au mojawapo ya JIJI la kusafiriwa mithili ya miji mingine mikubwa nchini.
ReplyDeleteNawatakia kila la kheri wananchi na viongozi wa wote wa Mkoa huo na wilaya zake pamoja na vitongoji vyake vyote. Keep it up in terms of development in all aspects in your Region and Nation at large. Nawatakia mkutano wa kheri, salama na amani.
we zebedayo huwa unaboa mno watu wakiongea ukweli, unajidai kuongea pumba zako ati kisa mzawa, kwani we mwenyewe ndo mzawa wa bongo? kama kuna mapungufu yasiongelewe? na kama kwa wenzetu kuna maendeleo bila ya ufisadi uliokubuhu tusiseme? kujidai tu msema kweli kumbe una nidhamu ya uoga. grow up!
ReplyDeleteHata kama ingekua UPDP ipo madarakani ingejenga barabara coz ndio majukumu ya serikali husika, hii ni sawa na mzee kumpatia mwanae mahitaji muhimu tu...
ReplyDeleteWadau wengi wanasahau kwamba sio tu tangu enzi ya uhuru bali tangu enzi ya mkoloni mjerumani kulijengwa reli iliyounganisha Kigoma na bandari ya Dar es Salaam, pengine ingejengwa nyingine kama "dili" ya AGRISOL Energy, IOWA State university na Serengeti Advisors isingepingwa na wanaharakati. Hivyo kwa mujibu wa wao hamna haki ya kuhoji hata kama ikichukua miaka 98 tangu ilipokamilika reli ya kati toka Dar hadi Kigoma hadi hii leo kutokamilika kwa rami inayounganisha Dar hadi Kigoma msihoji sababu mtaonekana mna wivu!
ReplyDeleteTusubiri tuone na hivi bajeti zenyewe tegemezi nadhani tutaendelea kungoja sana maana siasa imeingia hadi B.O.T kwenye wapanga sera na kusimamia uchumi. All in all naweza sema msukumo wa opposition parties kuanzia enzi ya kina Kabouru hadi hii ya leo angalau kuna dalili za uhai Kigoma na si kama ilivyokua kabla ya 1994 maana huko ni yale maendeleo yaliyoletwa na wakoloni hasa Wajerumani tu na bado bila aibu wapo wanaojivunia...
vitu kama barabara ni Serikali inajenga au CCM? Wanachi wote tunalipa kodi
ReplyDeletejamani wale vijana wa "kigoma stars" wameimba kweli kuwa kuna maendeleo kigoma. ninachoona kuwa wameimba ili watu watanzania wajue maana kuna tendency ya kuudharau mkoa wa kigoma. Imagine group yote hiyo ya vijana ni wa asili ya kigoma na wameamua kuuimbia mkoa wao. Big up!
ReplyDelete