Mmoja wa waasisi wa klabu ya michezo na burudani ya Tazara, Franco Kabigi (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam.
Franco, atakumbukwa kwa mengi ikiwa ni pamoja na kuwa afisa mwandamizi katika Studio za Sunrise mtaa wa Jamhuri jijini Dar es salaam na pia meneja wa zamani wa kampuni ya burudani ya Space 1900.
Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Mbagala Zakheem jirani na Kizuiani, na mazishi yanategemewa kufanyika siku ya Ijumaa katika makaburi ya Kinondoni.
Mola aiweke mahali pema peponi
roho ya Marehemu Franco Kabigi.
Mola aiweke mahali pema peponi
roho ya Marehemu Franco Kabigi.
- AMINA
R.I.P Franco ulikuwa kaka yetu kinondoni shamba mitaa yote around Tazara, Ada Estate na Galu street.
ReplyDeletei have lost an uncle, he was such a great guy! very sincere inlaw, shall miss him with my family.jibe
ReplyDeleteJamani Franco nimepata shock ya mwaka siwezi kukusahau kabsia katika maisha yangu yani nakukumba kwa mengi enzi ya YMCA, Studio Sunrise,Tazara nk. Michuzi partner amekwenda kumbuka mulikotoka naye enzi za Disco la YMCA security man and mpiga picha. Wapi Mallya, Sisco na wenzie.
ReplyDeleteMungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Michuzi tupe updates za mazishi yake plse na picha ikiwezekana huyu mtu alikuwa wa muhimu sana hapa Dar.