Mmoja wa waasisi wa klabu ya michezo na burudani ya Tazara, Franco Kabigi (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam. 
Franco, atakumbukwa kwa mengi ikiwa ni pamoja na kuwa afisa mwandamizi katika Studio za Sunrise mtaa wa Jamhuri jijini Dar es salaam na pia meneja wa zamani wa kampuni ya burudani ya Space 1900.

Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Mbagala Zakheem jirani na Kizuiani, na mazishi yanategemewa kufanyika siku ya Ijumaa katika makaburi ya Kinondoni.


Mola aiweke mahali pema peponi 
roho ya Marehemu Franco Kabigi.
- AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2012

    R.I.P Franco ulikuwa kaka yetu kinondoni shamba mitaa yote around Tazara, Ada Estate na Galu street.

    ReplyDelete
  2. mwanjila jbJuly 25, 2012

    i have lost an uncle, he was such a great guy! very sincere inlaw, shall miss him with my family.jibe

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2012

    Jamani Franco nimepata shock ya mwaka siwezi kukusahau kabsia katika maisha yangu yani nakukumba kwa mengi enzi ya YMCA, Studio Sunrise,Tazara nk. Michuzi partner amekwenda kumbuka mulikotoka naye enzi za Disco la YMCA security man and mpiga picha. Wapi Mallya, Sisco na wenzie.

    Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

    Michuzi tupe updates za mazishi yake plse na picha ikiwezekana huyu mtu alikuwa wa muhimu sana hapa Dar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...