NMB kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea yakiwa ni kujenga nyumba,kusomesha watoto na kufikia malengo mengine muhimu maishani mwao, ilizindua promosheni inayowezesha wateja wa NMB Bonus Account an NMB Junior Account kuingia kwenye droo ya kushinda tani ya saruji,mabati ya kuwezeka,amana maradufu,ada za shule,fulana za NMB pamoja na mabegi ya shule kupitia promosheni ya Jenga maisha yako na NMB. 


Hivyo basi, leo droo ya Jenga maisha yako na NMB imechezeshwa na washindi zaidi ya 167 wamejishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tani za seruji na mabati ya kuwezekea.



Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akifafanua jambo wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mineja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Sadiki Elimsu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mawasiliani wa NMB,Josephine Kulwa alisema “NMB inaamini promosheni hii sio tu kwamba itaongeza tabia ya kujiwekea akiba lakini pia itasaidia wateja watakaoshinda kufikia malengo waliojiwekea na pia kuboresha maisha yao”

Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akifafanua jambo wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mineja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia.
Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akibonyeza kitufe kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, sadiki Elimsu na Meneja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia.

Wateja wote watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye NMB Bonus Account au NMB Junior Account watapata riba ya kuvutia ambayo inaweza kuwa hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana zilizowekwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2012

    Sadiki Elimsu alikuwa kipanga wa Commerce na Bookkeeping tulipokuwa Tambaza Sekondari. Nakumbuka alikuwa mwanafunzi bora kwa mwaka wake katika masomo hayo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...