Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe(kulia) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Joram Biswaro(Katikati) wakati wa kikao maalimu cha nchi za Maziwa Makuu kilichofanyika sambamba na Mkutano wa 19 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika AU jijini Addis Ababa Ethiopia
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Sudan Omar Hassan el  Bashir wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika unaoendelea jijini Addis Ababa Ethiopia.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wanchi  za Afrika wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 19 wa wakuu wan chi za umoja wa Afrika(AU) jijini Addis Ababa Ethiopia leo. 
Picha na mdau  Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2012

    Hawa viongozi wa Afrika wanavaa suti za gharama gharama wakati asimilia kubwa ya wanaowangoza wanatembea uchi au madabwada.
    Mtoto wa Kabwela,Sweden.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2012

    JK omba mwongozo kuhusu vurugu zilizoko Mali,AU imekaa kimya sana..lakini kuwa makini usije kutolewa nje ya Ukumbi!

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2012

    We unasema nini?Mali kunatuhusu nini sisi wabongo?Tuliyonayo hatuyawezi halafu tutafute mengine,kuna fukara akatoa sadaka?Mm napinga any initiative yakupeleka msaada wa namna yyt Mali na Somalia kwani huko nikuingiza nchi kny mgogoro na jamaa ambao wanaitingisha USA na dunia kwa ujumla ALQAEDA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2012

    Mdau wa kwanza unalalamika nini kuhusu viongozi kuvaa suti kali. Ingekuwa wewe ungeacha kuvaa vizuri wakati mshahara unaruhusu? Acha ushamba. Hatuwezi kuwa sawa hata siku moja.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2012

    nilijua hutoweka comment yangu kila nikibeza anayekufadhili kununua hii camera yako canon sawa michuzi endelea hivyo hivyo lakini ujue tumeshachoka na vi tiripi vya mafisadi wenzako kwenda nje kila siku kwa kula kodi za wananchi pamoja na wewe unadhani hatulijui hilo kila kitu kina mwisho wake pondeni maisha lakini kaa mkijua ramadhan inakuja muumbeni sana mungu akusameheni maovu vyenu


    na hii pia usiweke

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...