1. Ndege mpya ya Precision Air aina ya Boeing 737-300 ikiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere tayari kwa kufanya safari yake ya kwanza kuelekea Lusaka, Zambia kupitia Lubumbashi – Congo DRC mapema leo.
1. Taswira ya ndani ya Boeing 737-300 iliyowasili wiki iliyopita toka Nairobi, Kenya ilipokuwa ikibadilishwa muonekano wake kwa kupakwa rangi za Precision Air, pamoja na kuipatia kibali cha kuruka katika anga za Tanzania na kimataifa pia.
1. Sehemu ya mkia wa ndege hiyo inayo onyesha usajili wake nambari 5H-PKS. Precision Air pia ina ndege Boeing 737-300 mbili zingine zenye usajili 5H-PMS na 5H-PAZ. Kwa ujumla sasa shirika hilo la ndege 12; ATR 72-500 tano, ATR 42 -500 mbili, ATR 42 -320 mbili na B737 -300 tatu.
Mbuni wetu yule asiyeruka sawa sawa (ATC) ni wakati sasa tumkabidhi kwa Mfugaji mahiri ili naye aweze kuruka sawasawa!
ReplyDeleteNi ajabu na ukweli ya kuwa Mbuni wetu tumekuwa nae chini ya usimamizi wa kundi zima la Kijiji chetu lakini ameshindwa kabisa kuruka kwa mbawa zake mwenyewe!
Sasa kuna ubaya gani tukamkabidhi Mbuni wetu kwa Mfugani mmoja fundi badala ya sisi Kijiji kizima kumfuga bila mafanikio?
Si ndio mnavyoona ndege anayefugwa na Mtu binafsi kama huyu PRECISON AIR ana mafanikio?