Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo katika Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(wapili kushoto), balozi wa jumuiya ya ulaya nchini Cerian Philberto Sebregondi(kushoto),Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji safi na mazingira Mjini Mbeya leo mchana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Kamishna wa Maendeleo katika jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs wafunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa MRADI WA MAJI SAFI na usafi wa mazingira katika eneo la Swaya mjni Mbeya leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(Watau kushoto) na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakikagua chanzo cha maji eneo la Swaya mjini Mbeya wakati wa uzinduzi wa mradi maji safi na mazingira mjni humo leo mchana.Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.


Kusoma hotuba ya Rais Kikwete BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    Tanzania Songa Mbele!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2012

    Nimesikia na kusikitika kuwa uhai wa mradi huu ni mpaka 2016! Kama niko sahihi usanifu wa miradi wa kipindi kifupi namna hii ni hasara kwa kuwa kutokana na ukuaji wa miji yetu ni uhai mfupi sana na muda si mrefu itakuwa kero tena. Itakuwa kama lile bomba la gesi la Songosongo ambalo kwa sasa linafanyia ukarabati mana ujazo wake haukidhi mahitaji ya gesi ya sasa!

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...