Mtanzania Rajabu Maoja bondia mzoefu katika ngumi za kulipwa kutoka mkoa wa Tanga atapanda ulingoni Septemba 1 kupimana ubavu na bondia Gottlieb Ndokosho bingwa wa ngumi nchini Namibia.

Mpambano huo unaofanyika katika jiji na Windhoek, nchini Namibia unawakutanisha mabondia wawili ambao wanazimudu vizuri ngumi ulingoni. Hii ni mara ya kwanza kwa bondia wa Kitanzania kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika nje ya nchi tangu mpambano katia ya Iraq Hudu na Ali Said wa Kenya ulivyofanyika jijini Mombasa mwaka 2000.

Wawili hao wataumana kwenye mpambano uliopewa jina la “The Battle for the Kalahari Desert” (Vita ya Jangwa la Kalahari) na waandaaji wa mpambano huo ambao ni Kinda Boxing Promotion chini ya promota Simon Nangolo wa nchi ya Namibia. Namibia iko Kusini Magharibi mwa bara la Afrika ikikingana na Afrika ya Kusini, Botswana na Angola.

Mtanzania Rajabu maoja anatokea katika jiji la tanga na ni mkali aliyejijengea umaarufu mkubwa katika masumbi hapa nchini. Maoja ni kati ya mabondia wachache wenye majina yanayotishia maisha baadhi ya mabondia wenzake katuka bara la Afrika.

Katika uhai wake wa ngumi Maoja amepigana mapambano 31 akishinda 18 na kupoteza kwa kiduchu mapambano 10 ambayo mengi sio yenye hadhi yoyote ya kumharibia historia yake kwemey ngumi na kutoka sare mapmbano matatu (3)

Naye bondia Gottlieb Ndokosho ambaye ni bingwa wa Namibia amepigana pambano 15 na kushinda 11 wakati amepoteza mapambano 3.

Mpambano huo uliopewa jina la The Battle for the Kalahari Desert (Vita ya jangwa la Kalahari) utasimamiwa na Rais wa Shirikiso la ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Aidha Ngowi ndiye Rais w kamiehsni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) na mkurugenzi wa ngumi wa baraza la Ngumi la Jumuiya ya madola.

Watanzania, tumuezi mwenzetu rajabu maoja anapopeperusha bendera ya Tanzania. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Imetumwa na;

Onesmo Ngowi
Rais wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi
Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)
Mkurrugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2012

    anatakiwa ajenge mwili na anyoe hizo nywele zake za tumbo na kifua kwani ni diskas

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2012

    DU NDIO KWANZA LEO NAMSIKIA HUYU BONDIA WA HAPA NYUMBANI PAMOJA NA HISTORIA YAKE HIYO ULIOYOTUDOKEZA NDUGU MWANDISHI

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2012

    Mmh! Mtawajua tu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2012

    Wewe unayetaka bondia anyoe nywele zake za kifua, unataka akuchumbie? kwani amesema yuko hapa kutafuta mke? au wewe ni mkewe wa zamani?

    ReplyDelete
  5. Kila la heri bondia wetu.
    Next time msikubali jina kama hilo, kwa sababu tayari unampa nguvu na ujasiri zaidi bondia wa Namibia unaposema "the battle for Kalahari desert" sasa mtanzania apiganie Kalahari ya nini kwake? ila mnabibia ana kila sababu ya kupigania Kalahari.
    Anyway, kila la heri.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2012

    kweli hata mimi nimesitushwa na huyu jamaa mwenye ushauri wa kunyoa nywele za kifuani, mke wangu mbona anazipenda sana nywele zangu za kifuani,mwenyewe anazipapasaga kila usiku,sasa wewe ndugu duh !!! au labda uko huko UK au USA huko nasikia kuwa shoga sasa hivi ni ruksa mpaka makanisani !!! wewe achana kabisa na nywele zetu za kifuani. Zebedayo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2012

    Huyu muuza sura bondia anapiga picha mikono mavumbi minywele kifuani hata sio presentable... ipo kazi mweh.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2012

    namunga mkona mdau wa hapo juu aliyesema jamaa anyowe hizo nywele au kama hawezi basi azipare pare azichane chana because ziesokotana kama vijinzi viluwi luwi vidogo vidogo jaama haoni hata haya kukaa hivyo angekuwa na singa singependeza kama za kizungu zungu haaaaaaaaaaaaaaaaaa

    nyowe wewe mbaba au huna kiwembe njo nikuazime kiwembe changu cha mashine ya umeme moto moto moto moto eeeh

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2012

    hawa wanao-comment kuhusu kunyoa hiyo garden love kama ni wanamume..basi watakuwa wana walakini fulani. hivi zinakusumbueni nini hizo nywele? angalieni....jamaa mtoto wa ki-Tanga huyo...ohooooo!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2012

    hatuna walakin wowote bwana ila kama vinapendeza nikitunzwa na kuchanywa chanwa vizuri kama hapo juu jamaa aliyesema mama anazikuna kuna kila usiku kwa sababu zimetunzwa vizuri lakin zikiwa kama za huyu jamaa AISE NOMA KICHIZI KIYAMA.
    Kama ujuavyo sisi wabongo nywele zetu si singa kama wenzetu halafu basi tuziweke ovyo ovyo si balaa hili

    mimi mwenyewe nina nywele hata miguni lakin nazituza fresh na summer time nazinyoa kwa sababu joto kiyama huku nilipo sitaki ninuke nuke nazoo

    so hatuna kasoro zozote tunavyo mwambia azinyowe kama akishindwa kuzitunza kuzichana chana na kuzipaka mafuta zingare alright mkuu

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2012

    kata hayo manywele wewe,utadhani umeweka uchi wa mwanamke kifuani.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 22, 2012

    ANAWA MIKONO HALAFU ANGEVAA TISHETI TU. KIFUA WAZI NOMAA

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 22, 2012

    Hapo kifuani utadhani wametuwa nzi, pamekuwa ni attraction ya macho ya watu in negative way. Mmoja wetu hapo juu kajisemea...alau angekuwa na singa zingependeza kama za kizungu zungu..., ni kweli Anon. Lakini hiyo kipilipili kijana, haipendezi, jaribu kukivalia japo fulana au t-shirt mbele za watu, ukiwa kwako ruksa, full kujiachia, lakini sio kadamnasi ya watu (ni ushauri tu, don't take it personal).

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 22, 2012

    Duh! Hizo zinazoonekana ziko hivyo, sasa zile ambazo hazionejani si balaa???? Ha ha ha haaaaaaaa! Kweli bunadamu tuko kila dizaini na hizi nguo huficha mengi.....

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2012

    hajaoga huyo...mchafuu!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...