Kwa niaba ya ccm tawi la afrika ya kusini, tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya meli ya MV SKAGIT, iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar kuelekea zanzibar, ambayo imesababisha wenzentu wengi kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Tunawapongeza na kuwashukuru taasis mbali-mbali na watu binafsi wanaofanya kazi kubwa kukabili zoezi la uokoaji, na wale waliotufikishia habari hizi. tunawashukuru wale wote waliopata taarifa na kuelekea kwenye eneo la tukio na kuanza ukoaji mara moja.
Uongozi wa tawi la ccm afrika ya kusini, tuko pamoja nanyi, pia tunaungana na watanzania wenzetu wote kutoa pole kwa wafiwa, na kuwaombea majeruhi waweze kupona kwa haraka.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote nakuwapa nguvu na uvumulivu ndugu na jamaa, katika kipindi hiki kigumu.
Paul PA Koba
Katibu Mkuu,
CCM Tawi la Afrika ya Kusini.
amen, Mungu atatutia Nguvu.
ReplyDelete