Bwana Michuzi pole sana na safari na natumai hio fufu unaila wakati wa daku na si lanchi.

Baada ya kufuliliza kwa ajali wiki hii nimeona niombe uniwekee mchango  wangu huu mdogo labda utaweza kusaidia japo kiduchu kupunguza ajali.
 
Najua waswahili tunasema ajali haina kinga ila kuna pointi mbili tatu tukizizingatia inaweza kuongeza umakini.
1. Kila dereva wa basi alazimishwe kubandika copy ya rangi iliyokuzwa (A4) ya leseni yake ya udereva nyuma ya kiti ili abiria waweze kumtambua na kuwa na uhakika na sifa zake za udereva. Wakati wote wa Safari awe amevaa leseni yake orijino shingoni.

2. Kila basi liwe lina namba yake ya usajili VIN (kama TIN) na ibandikwe kubwa ubavuni na ndani ili liweze kutambulika kiurahisi. 

3. Habari zote zinazolihusu basi lililosajiliwa ziwekwe kwenye mtandao na ni jukumu la mmiliki kuupdate habari hizo kila baada ya muda fulani.

4. Kuwe na namba maalumu (short code) mfano 155XX ambayo mwananchi au abiria ataweza kuripoti kwa sms kama hapendezewi na uendeshaji wa dereva kwa kutaja VIN ya basi hilo na ruti yake hivyo kuwawezesha traffic kufuatilia.

5. Kampuni za simu zijitolee meseji zote kwenda namba hio ziwe ni bure

6. Tuwe na road marshals (mfano wa air marshals), maafisa wa Sumatra ambao kazi yao ni kusafiri na mabasi na kuripoti yale yanayovunja sheria. Uvunjaji wa sheria unaweza kurikodiwa (sauti au video) kwa kutumia smart phones.

7. Najua Rushwa ni adui yetu mkubwa lakini uwepo mpango wa kutoa kamisheni kwa maafisa husikakwa kila kosa litakalotozwa faini

Vitu hivi vichache vinatekelezeka katika kipindi kifupi sana,tungeanza na haya wakati tukiendelea na mikakati kabambe ya kupunguza ajali. Tunaweza kuanza na mabasi ya mikoani halafu madaladala, bajaji na bodaboda zikafuata.

Natanguliza shukurani zangu. Wako katika ujenzi wa Taifa

Mdau
Che

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Naam, Mdau CHE wazo lako zuri lkn point zako zote hazina maana umekuja na solution moja kwa moja bila kuangalia vyanzo vya ajali kwanza. Nikurudishe form one ambapo tulisoma scientific methods of solving problems, ni kama ifuatavyo MOSI kugundua tatizo, PILI kulifanyia kazi hilo tatizo na kulipatia jibu rahisi la kubuni, TATU jaribio, NNE jawabu, TANO hitimisho na jinsi ya kulitatua, nimeelezea kiuchache zaidi na kwa kukatisha.

    Sasa basi kutokana na ajali za mara kwa mara utafiti wa kina inabidi ufanyike na mamlaka husika sio kukurupuka tu na solutions zako amabazo hazina kichwa wala miguu.
    Kama gharama za uchunguzi ni kubwa kwa kuanzia yafuatayo yafanyiwe kazi haraka MOSI madereva wapatiwe elimu hata kwa mkopo ili wawe na taaluma za kutosha, PILI Mabasi yafanyiwe uchunguzi kila baada ya miezi situ kama ni salama kusafirisha abiria bila kuleta madhara kwa watumiaji wengine wa barabara na TATU kama tunavyoona kuwa kuna namba za trafic officers basi ziwekwe kwenye tickets za abiria na hapa ziwe za kila check point kwa mfano derava akipita traffic check point ya kwanza akileta upuuzi abiria wanapiga simu check point ya mbele then anashughulikwa na adhabu iwe adhabu sio atoe hongo mchezo uishe kimtindo huo.

    Ebana ee kuna mengi ya kuandika naona wadau wengine waongezee hapo.

    Mdau UK.

    ReplyDelete
  2. Mdau umejitahidi kutoa viangalizo ili kupunguza ajali. Viangalizo vyako ni sahihi lakini umesahau pia aina za barabara tulizo nazo kuwa ni chanzo kikubwa cha ajali. Barabara zetu ni finyu (nyembamba) mno kwa magari kupishana. Pia barabara zetu zinapoharibika inawachukua muda mrefu wahusika kuzitengeneza. Mimi nimekuwa nikitoa ushauri kila mara kuwa barabara zetu hasa "highways" ziwe mbili zenye "lanes" hata tatu au nne kila moja. Hii itasaidia kupunguza mwingiliano wa magari yanayokwenda na yanayorudi.

    ReplyDelete
  3. Mdau amesema ukweli. Ila ningependa kuongezea kuwa AJALI INAYO KINGA. si kweli kuwa ajali haina kinga....AJALI INA KINGA. Kama kila mtu hasa madereva watakuwa makini hizi ajali hazitakuwepo hata moja. Mimi nimeendesha miaka 15 hapa Canada sijaona ajali kwenye barabara nayopita kwenda kazini (mile 25 jumla mile 50 kwenda na kurudi na kuendesha mile 250 wikiendi) Ankal Michuzi ningependa kushauri tu kwamba solution kubwa ni kujenga dual lane barabara zote kubwa zinazounganisha mikoa la sivyo siku zote tutakuwa na hilo tatizo. Pia polisi waache kuchukua rushwa kuruhusu magari mabovu kutembea. Najua uko huko Accra na JK, please mweleze JK kuwa wananchi wake hatutaki kuona watu wanateketea. WANANCHI WATAKUFA HADI LINI.

    ReplyDelete
  4. nazani wewe unataka kuwatengenezea watu ulaji,yaani rushwa kwa kifupi hiyo serikali haijali kuhusu ajali sababu wenyewe na familia zao hawapandi mabasi

    ReplyDelete
  5. Mdau Che mawazo yako ni mazuri sana lakini tatizo tulilonalo watu wenye mawazo kama yako hawapo SIRIKALINI, Na hata kama wapo wanashindwa kutekeleza argenda nzuri na zenye faida kwa taifa kwa kua wachahe wenye uchu hawajali mwananchi wa kawaida isipokua ni kujinufaisha wao. MICH USIBANIE HII TAFADHALI.

    ReplyDelete
  6. Mdau nakupongeza sana sana kwa maoni yako hata hivyo kama mdau wa usafiri nchini kila dereva wa basi la masafa huwa na cheti chake tena ORIGINAL ndani ya basi sawia na leseni yake na kutokuwa na vitu hivyo ni kosa na hukaguliwa kila wakati na trafiic.

    Code no. za polisi zipo na hutolewa ktk magazeti mbalimbali ili raia waweze kuwasiliana na Jeshi ikiwa kutatokea tatizo bali umuhimu wa makampuni ya simu kujitolea hapo SAWA KABISA.

    Maafisa wa SUMATRA husafiri na mabasi ambayo yametolewa taarifa na abiria au pale wanapohisi kuvunjwa kwa masharti mbalimbali ya leseni.

    Binafsi ningeomba kupata email yako.

    Asante

    ReplyDelete
  7. SAFI SANA; ILA SINA UHAKIKA KAMA KWA HII BONGO YETU WATASIKILIZA. WATU WAGUMU WA KUELEWA; WEPESI WA KUSAHA; WARASIMU WAKUBWA. ILA MCHANGO MZURI SANA NA KAMA UTAFUATILIWA UTASIMAMIA.

    ReplyDelete
  8. Mdau Che nakubaliana nawe. Ingawa hiyo namba 6 ya road marshals hao watakuwa wanakula rushwa tuu.

    ReplyDelete
  9. Mdau Che,

    Wazo lako ni zuri sana !

    La ziada No.8 Madereva wote wawe na Kadi za uangalizi wa mwenendo wa afya zao kama zilivyo kadi za Kliniki kwa akina mama wazazi na watoto wachanga.

    Kadi hizo pia zibandikwe kwenye kiti au ndani ya basi ili abiria wathibitishe ya kuwa wanahudumiwa na Dereva mwenye afya isiyo mgogoro na akili timamu.

    Kwa sababu afya ya binaadamu haina dhamana inaweza kuimarika ama kutetereka wakati wowote.

    Bahati mbaya sana haswa kwa Tanzania taratibu za vipimo hazizingatiwi na zinafanywa kwa kulipua.

    Ndio maana unaweza kukuta mtu ni un-fit kuendesha labda macho yake yana nguvu ndogo au yamekufa kabisa lakini anahonga anapata cheti cha macho anachukia Leseni ya Udereva.

    Kwa uendeshaji wao wa ajabu hasa Madereva wa mabasi inawezekana kabisa mtu aliipataLeseni akiwa mzima lakini kwa ajili ya mabangi yao akawa ameshafyatuka na ni Chizi fresh na yupo kwenye usukani.

    Je kwa mtaji huo hapo wa madereva wasio na afya njema kama machizi kweli tutapona?

    Na je wimbi la ajali litapungua???

    ReplyDelete
  10. Mdau Che,

    Kutokana na mabangi ya madereva wengi hasa wa mabasi mijini.

    No.8 wawe wanapimwa akili kila baada ya miezi mitatu na rekodi ya vyeti inawekwa nyuma ya kiti cha Dereva!

    ReplyDelete
  11. Dereva Makini TzAugust 11, 2012

    Wewe unasema sisi madereva tunakula Bange? anaekula Bange baba yako mzazi! pambaf.

    Siku zenu za kufa zikifika mnatulaumu sie? sie tunafanikisha tu vifo vyenu kwani ni mipango ya Mola.

    Mnataka sisi tuzuie mipango ya mola?

    Pambaf nyote hapo juu

    ReplyDelete
  12. Wote mna mawazo mazuri lakini bado hamjasema chanzo cha ajali,nadhani ajali zinatokea kwa sababu ya leseni za udereva zinazotolewa bila utaratibu,learner ukienda TRA unalipia na unaondoka nayo bila kufanya mtihani wa alama za barabarani,leseni ni pesa yako,hakuna kufanyishwa mtihani wa kuendesha.Na la kushangaza zaidi kuna hata madereva wasiojua kusoma wala kuandika.Mimi ningependekeza vianzishe vyuo vya madereva wa ma bus na mizigo katika kila kanda ya Tanzania na kiundwe chombo cha kutoa leseni za udereva ambacho ni tofauti na jeshi la polisi.

    Sugu

    ReplyDelete
  13. Huyo Mola ndie aliyekwambia atatutoa duniani kupitia nyie madereve?

    ReplyDelete
  14. Swala kubwa ni kufanya research ya Tatizo na kufuata taratibu.Mimi huwa nasafiri mwendo mrefu sana toka dar-es-salaam lakini sijawahi kusafiri nikashindwa kuona madereva wakitoa pesa kwa matrafic na sehemu nyingine ni kawaida na kama utamaduni wao hata kama hawana makosa wanakuwa kama ni mchango fulani wanatoa.Haya matatizo yanahitaji solutions za idara mbalimbali na si idara moja tu pia linahitaji uzalendo wa hali ya juu hivyo tunahitaji cooperation ya hali ya juu ili kuondoa tatizo hili ila pia ujue haya maswala yanategemea level ya maendeleo na civilization ya jamii husika.

    ReplyDelete
  15. Mdau Anonymous wa Sat Aug 11, 11:50:00 AM 2012

    ...unarukia kwenye matusi kutukana baba wa wengine.

    kama imependekezwa Madereva wapimwe va vyeti viwe nyuma ya kiti, WEWE KWA KICHAA CHAKO UPIMWE NA CHETI CHAKO TENA CHENYE PICHA KITUNDIKWE HUMU KWENYE BLOGU KWA MICHUZI.

    USIKATAE KITU BILA UTAFITI, KAMA UNABISHA KAMA BAADHI YA MADEREVA HAWAHUSIANI NA MATUMIZI YA BANGE NENDA MAKAO MAKUU TA TRAFIKI UKAULIZE UELEZWE RIPOTI KABILI ,PALE WANAZO REKODI NA DATA, KWA TAARIFA YAKO AJALI NYINGI ZINALETWA NA BAADHI YA MADEREVA WASIO MAKINI WANAOTUMIA HAYO HAYO MABANGE UNAYOKATAA WEWE.

    CHANGIA MAWAZO YA KUJENGA NA SIO KUBOMOA!

    ReplyDelete
  16. wazo zuri.
    nirudi kwa anonymous aliyeanza kwa kuandika nadharia nyiiiingi alizofundishwa "primary". Wewe ndio mfano wa walio wengi serikali, ni wazuri katika kukariri nadharia mlizofundishwa na wazungu, ukapata "A" kwa ajili ya kukakariri ukajiona umeelimika. Penye hizo nadharia na wenye first class degree kwa ajili ya kuzikariri kisha zikawa hazikufanyiwa vitendo ni sawa na mkono mtupu..... Narudi kwa ndugu yangu Che, mawazo yako ni mazuri tena sana, tunahitaji watu wenye straight solutions that can be implemented badala ya kutumia theory nyiiingi kuweka kamati, makongamano na vikao vya kujadili hizi theory kisha waje na conclusion kuwa ni za primary hivyo hazifai kutumika. wakati huo wanakuwa wametumia fedha ya walipa kodi.
    WAZO BINAFSI: tanzania inahitaji viongozi ambao ntawaita "madikteta wa maendeleo" ambao badala ya kusikiliza maneno mengi ya akina anonymous, wawe wanasikiliza maneno ya wachache wenye straight solutions, kisha zikawa implemented.
    Big up Che..

    ReplyDelete
  17. Ajali zote hizi ni matokeo ya rushwa na uiongozi dhaifu katika kila taasisi. Suala la ajali nchini linahitaji ushirikiano wa taasisi zaidi ya moja. Je ziko tayari kisaikilogia, kitaalam na kiushirikianao kupunguza au kumaliza tatizo hili? Fanya lolote lakini kama hakuna uongozi bora na makini sahau!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. Mdau wa kwanza shukurani kwa mchango wako, tafiti,solutions na proposals ziko kibao zinajaa vumbi Wizarani. Mimi nimetaja solution za muda mfupi, kujenga lanes, kutrain madereva, kupima mabasi hizo zote ni za muda mrefu ambazo zitahitaji bajeti ya kueleweka. Short code from TCRA na makubaliano na kampuni za simu vinapatikana in two weeks. Ongeza wiki mbili zaidi madereva kukamilisha vinayowahusu na Sumatra kujipanga na ndani ya mwezi tunaanza zoezi.
    Mdau wa Sumatra, kwanza namba za simu ziwe short codes rahisi abiria kuzishika na ziwe visible kwenye basi sio kwenye magazeti, Dereva avae leseni shingoni na nyuma ya kiti chake ili abiria aione na si mkaguzi au traffic, hao marshals wapande mabasi yote randomly na si kungoja kuambiwa na cha muhimu ni kuongea na Wizara ya Fedha wawaruhusu Idara ya Usalama Barabarani kubaki na sehemu ya mapato kama motisha kwa traffic.
    Che

    ReplyDelete
  19. Michuzi kwa nini unaruhusu watu wasio wastaarabu kwenye blog yako? Wachangiaji wanatoa comments za maana wengine kama huyo hapo anon wa saturday 11,10.50 am anaropoka matusi bila hata kujali wasomaji wenye busara. Sijui amefundishwa na nani anaposema wao wanafanikisha vifo vya watanzania kwa sababu vimeandikwa na mola, je aliona hicho kitabu kilichoandikwa siku za watu kufa? asilete imani yake kwa watu wote ili awafanye waamini. Michuzi watu wafuate sheria na hizi ajali zitaisha kama si kupungua sana, Barabara zetu hazina hata sehemu za kuonyesha wapi ni daraja, kona au mwendo unaotakiwa kuendesha.....sasa ajali zitapungua kwa jinsi hii? Tufuate sheria na atakayesababisha ajali anapaswa apelekwe mahakama na afungwe bila kujali ni waziri au tajiri....haki kwa wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...