Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akimkabidhi kadi ya CHADEMA aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo jimbo la Mvomero, bwana Charles Kiwaga. Wengine ni wanachama wapya wa CHADEMA tawi la Kododo Mvomero. 

Operesheni Sangara inayoendelea kwa upande wa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Bwana Deogratias Munishi amezidi naye kupasua vijiji ndani ya Mvomero, Morogoro. Pia wanavijiji walimuonyesha hali halisi ya maendeleo katika kata yao ya Luale kwa kipindi kirefu walichokuwa chini ya CCM tangu miaka 50 iliyopita mpaka sasa na wakiwa wamekata shauri kujiunga na CHADEMA kama chachu ya mabadiliko.
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM kata ya Muhonda akieleza jinsi alivyokunwa na sera za CHADEMA zilizoelezwa na katibu Mkuu wa BAVICHA katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kichangani.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akikabidhiwa kadi na sare za CCM kutoka kwa katibu mwenezi wa kata ya Muhonda Jimbo la Mvomero, Mzee Ngoya.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akikagua majengo ya shule ya msingi Kododo kata ya Luale jimbo la Mvomero. Shule hii ina wanafunzi 652 na mwalimu mmoja tu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. safi sana CHADEMA ,wananchi na watanzania wenye uchungu na maendeleo badilikeni na 2015 fanyeni mabadiliko kwa ajili ya maendeleo yenu kwa kuichagua CHADEMA ,kwani CCM imepoteza mwelekeo na ni zaidi ya miaka 50 baada ya uhuru lakini umasikini unazidi na manufaa ya rasilimali za nchi zinanufaisha wachache.Madau big

    ReplyDelete
  2. mmmm!!! wanafunzi 652 mwalimu MMOJA ?????? hii habari mbona imekaa kama , you say ,he say. sijui ???Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  3. Angalau sasa mmeanza kutoa habari za Chadema baada ya kuwaeleza ukweli juzi.

    Soma alama za nyakati. Karibu Chadema inachukuwa utawala wa nchi.

    ReplyDelete
  4. Mzee ama kweli unazeeka vibaya!

    Huku ndio kuingia mkenge mazima!

    Yaani katika umri huo wa lala salama unahamia Chadema kutoka CCM wakati ni wazi hiyo miaka 50 unayodai hukupata maendeleo huwezi kuifikisha kutoka sasa!

    ReplyDelete
  5. Wewe Mzee wa CCM uliohamia CDM hujui hao jamaa wana Siasa zanye sera za mchezo wa Genge la 'Karata tatu' ???

    ReplyDelete
  6. Ohhhh Mzee umehama CCM kwenda CHADEMA umeshaukalia!!!

    Kwa kweli umeuziwa fisi ndani ya gunia ukiambiwa ni mbuzi.

    Kimkoa wewe upo Mvomero-Morogoro wakati chama hicho kina sera za Kanda ya Kasakazini Kilimanjaro na Kichagga!

    Enhee utakuwa Mhamasishaji maisha yako yote ndani ya Chadema.

    Sasa MOROGORO na KILIMANJARO wapi na wapi?

    ReplyDelete
  7. Katibu Mwenezi uliyehama CCM kwenda CDM, ama kweli 'umeukalia na umekatika' vibaya vibaya pamoja na uzee wako huo!

    Ina maana pamoja na umri wako huo unashindwa kutambua mbivu na mbichi?

    ReplyDelete
  8. Hawa wazee hawajaanza leo, alikuwepo mtu anaitwa shehe mtopea, yuko wapi sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...