Wizara ya Maliasili na Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake tisa (9) kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori Hai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa hatua husika kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.

(1) Waliofukuzwa kazi kutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:

(i) Bw. Obeid F. Mbangwa - Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Matumizi ya Wanyamapori,
(ii) Bw. Simon Charles Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,
(iii) Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.

(2) Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama ni:

(i) Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuia Ujangili.

(3) Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la Maandishi:

(i) Bibi Martha P. Msemo - Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.
(ii) Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.

(4) Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.

(i) Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.

(5) Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:

(i) Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori
(ii) Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.

Wahusika wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.

[MWISHO]

Mhe. Khamis Suedi Kagasheki
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII
13 Agosti 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. i thought summary dismissal was repealed by the Employment and Labour Relations Act,2004.,

    ReplyDelete
  2. Ndugu ukicheza na nyani utavuna mibua..pangua pangua..hakuna kulala..yaani yaje yakukute kwa hao wajinga..fanya kazi kutetea taifa lako..ongeza adhabu ili waogope kufanya manyago..muda simrefu ntakuweka kundi la...mwakiembe..magufuli..samweri sita...ujumbe kwa mwakiembe na magufuli..vip mbona kimiya daraja la kigamboni?..coz nawaaminia...ni mm tajiri wa mawazo endelevu..sikusoma ila naona mbali...amani kwa wadau wote.

    ReplyDelete
  3. Sioni hatua yoyote hapo. Kosa kama hilo mtu anafukuzwa kazi tu. au anapewa onyo. kwanini wasipelekwe mahakamani kama imeonekana na kuthibitka wametenda kosa kubwa kama hilo.
    Naona ni mwendelezo wa siasa zilezile za danganya toto.

    ReplyDelete
  4. Mh. Waziri, ni muda wa kuwarejesha maafisa walioacha kazi au kwenda kusoma ili kuepukana na uozo uliokuwepo hapo wizarani.

    ReplyDelete
  5. Wakola muno Ta' Kagasheki.Mungu akubele

    ReplyDelete
  6. Wakila muno Ta' ni nini? Andika kiswahili acha ulabila silly thing

    ReplyDelete
  7. sasa hao twiga ndio watarudi! au ndo danganya toto! kama imeshajulikana ulikuwa ni wizi basi hao wanyama warudishwe na hao walioiba wachukuliwe hatua! au twawaogopa waarab!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...