Habari za kazi 

Mimi ni mwanaume wa kitanzania, natafuta mchumba, awe ni binti wa kitanzania asiyezidi miaka 30. mkristu kama mwislamu awe tayari kubadili dini, asiwe mlevi wala mvuta sigara, awe hajawahi kuolewa wala kuzaa. 

Maombi yanakaribishwa kutoka sehemu yoyote duniani mradi ukidhi vigezo hapo juu. Mengine tutawasiliana zaidi. maombi yatumwe bkasimba@rocketmail.com. 

Niko serious no time wasters pls. ukituma na picha inakupa advantage zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Brother, Have a little respect to your mothers, Hivi unadhani mwanamke ni kama bidhaa vile ?!,hadi unafikiri kumnadi hapa,eti " ukituma na picha inakupa advantage zaidi !!", thats degradaation into your lowest self wickedness !!!,have a little respect to your sisters !!!, infact in the world of righteousness,they used to kill people like you for dis-respecting women like this !!!. Be careful brother !!!!, please !!!. If u r looking for a woman to marry, approach them in good manners,u know the procedures, u got your ndugus,wazee wako,watakufundisha jinsi gani ya kukamilisha jambo lako hilo zuri la kuoa if u r serious !!!. Peace :)

    ReplyDelete
  2. mbona wewe maelezo yako huyatoi

    ReplyDelete
  3. Ninavyojuwa mimi ni rahisi kumpata mkristo kubadili dini na kuingia uislam lakini kumpata muislam kuingia ukristo ni kazi sana maana dini ya kiislam sio kama chama cha siasa ni dini ya kweli

    Kwa ushauri wangu nenda kwenye yale majumba ya walokole utampata mwenye sifa ulizozitaja

    Mdau wa kanisa la kakobe.

    ReplyDelete
  4. UNAFANYA KAZI GANI? UNA NYUMBA? MAANA SIO TUKAWEKANE KWENYE NYUMBA ZA VYUMBA SITA,,HAYA NA UNA SHILINGI NGAPI KWENYE ACCOUNT YAKO?

    ReplyDelete
  5. Ovyooooooooooo..ww si ulizaliwa.sasa kwa nini useme hutaki aliezaa??kwani kuzaa dhambi?/no wonder hadi sasa hujapata hata rafiki unatafuta mitandaoni.na hutapata labda uumbe wa kwako

    ReplyDelete
  6. Katika dunia hii kama umeshindwa kumpata anayekufaa kati ya uliowaona kwa macho, sijui kama utaweza kwa mtandao.

    ReplyDelete
  7. Acha UTUTUSA wako! Kwani upo gerezani hadi unatumia mtandao kutafuta mchumba? ulikopita kote hukuona hadi utumie njia hii?

    Sura pia hujaona hadi sasa unataka za kuona picha? sidhani kama hapa kuna uzima

    ReplyDelete
  8. HABARI MDAU?MIMI NAKUSHAURI NENDA KWENYE UWANJA WA FISI WAREMBO KIBAO WANATAFUTA MCHUMBA KAMA WEWE ASANTE.MDAU NEWHAM.

    ReplyDelete
  9. mimi pia mwanaume natafuta baradhuli wa aina yoyote sina ubaguzi wa rangi wala dini asizidi urefu wa futi nne na inchi tatu picha sio muhimu sura ikiwezekana picha ianzie kiunoni mpaka kwenye kisigino,nitashukuru kama muhusika atakuwa mtu wa pwani pwani.
    kwa maelezo zaidi wasiliana nami kwa anuani hii.
    mzee busha mcheche.
    tandika,karibu na choo cha sirikali.{mikoroshini}
    ukiniulizia hapa kwa wazee wacheza bao utanipata.
    Daresalaam.
    kwa waliopo nje mtanisamehe nawaomba muhudumiwe na nchi za karibu yenu au ubalozini.
    asanteni.

    ReplyDelete
  10. Unatafuta Kibaraka wewe na si Mchumba

    ReplyDelete
  11. IT SOUNDS LIKE A JOB

    ReplyDelete

  12. Apewe jini baya huyu aliweke ndani, maana fitna huyu.

    ReplyDelete
  13. Ndugu Boss...Mimi ni binti wa miaka chini ya 30.Sinywi wala sivuti sigara bali navuta bangi.Sijawahi kuolewa wala kuzaa.Ninaishi Somalia kwa sasa ila kwetu Iraq.Siko tayari kuzaa sababu haiko kwenye vigezo vyako.Kwenye hyo picha yangu nadhani utanipenda....Umeona ninavojua shika AK 47??uko tayari??

    ReplyDelete
  14. Mwislamu hasa hasa si rahisi kumpata na akabadilisha. Ukimwona mwislamu anabadilisha dini kwa sababu ya kuolewa huyo si mwislamu hata akisali usiku kucha. Dini ya kiislamu sio karata bwana zinazochezewa bwana. Tafuta wagalatia wenzeko

    ReplyDelete
  15. baada ya kusoma maoni haya nimegundua kuna dini moja hapo ni wavumilivu na wastaarabu na dini nyingine dahh...!!!
    ila sijui ni ipi.

    ReplyDelete
  16. mimi nadhani nakufaa maana sinywi pombe wala sivuti sigara bali navuta bangi tu na kunywa gongo, sijaolewa bali naishi na bwana, sijazaa ila nimeadapti mtoto wa kike, nina umri chini ya 30, pia sio muislamu ila sina dini kabisa ........Ahsante kwa kujitokeza picha yangu utaiona kwa email yako..., ni mzuri sana na p[ia natumia karolight..!!!!!

    ReplyDelete
  17. Umeula wa chuya hutampata ng'ooo Mwanamke Mwislamu wa Kumritadisha katafute Mapagani wasio na Dini ndio uwaingize kwenye Ugalatia!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...