Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda
kuwataarifu kuwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura ameteuliwa na SZhirikisho
la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa watakaoshughulikia
masuala ya habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake
zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou
kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa fainali hizo za Mataifa ya Afrika
kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28, 2012 na kumalizika Novemba
11, 2012.
Wambura atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia
habari kwenye fainali hizo. Wengine ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF,
Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola.


Pumu imepata mkohozi.
ReplyDeleteNgoma imefika kwa kenge.
Upele umempata mkunaji.