Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akitoa hotuba yake katika hafla ya uzinduzi wa Ofisi mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya iliyopo mjini Kibaha.
Mkurugenzi wa NHIF, Emanuel Humba akitoa maelezo ya utangulizi ya Mfuko kwa wageni walioalikwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, Dk. Mpemba akitoa shukrani kwa Mfuko kwa ushirikiano wake katika uboreshaji wa huduma za matibabu katika hospitali ya Tumbi.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
Karibuni Pwani, matibabu hayo ni muhimu kwa sisi wananchi wa hapa.
ReplyDeleteNinakerwa sana na ninyi wanawake ambao MNATUMIA KEMIKALI au kwa lugha rahisi KUJICHUBUA. Yaani, hakuna cha uzuri wowote hapo hivi mlishawahi kutembelea mahospitali na kuona watu ambao wanapata taabu kwa sababu ya kemikali hizo hasa KANSA?
Kwa maoni yangu, mtu yeyote ambaye tunataka kumweka ashike nafasi ya juu kuongoza wananchi inabidi aangaliwe mara mbili, kwani kwa mtu anayetumia kemikali hafai kuwa kiongozi. Kwani, kiongozi ni kioo cha jamii. Nakumbuka miaka ya zamani serikali ilikuwa inafukuzana na AMBI, JARIBU; sijui leo hii iko wapi?