Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) akibadilishana hati ya mkopo wa shilingi bilioni 280 kutoka kwa Meneja Mkuu wa Benki ya Exim ya India Geeta Poojary (katikati) leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kusaidia usambzaji wa maji mji wa Chalinze na Jiji la Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa India Debnath Shaw.
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya india kupitia Benki ya Exim kuikopesha Tanzaniashilingi bilioni 280 kwa ajili kusaidia kusambza maji katika Jiji la dare s salaam na mji wa Chalinze. Kulia ni Meneja Mkuu wa Benki ya Exim ya India Geeta Poojary.
kila siku mnapewa mikopo kila siku na wao wanachukua rasilimali zetu nakwambia ndo maana nchi za africa haziendelei watu hawajasoma utawala na kama wamesoma basi wanajinufaisha vitambi vyao na familia zao ujinga ujinga kila siku
ReplyDeletemdau washingtona d.c
nilijua hutoweka comment yangu fisadi na wewe pia michuzi wa nchi hii yetu
ReplyDeleteHivi ninyi waandishi wa hizi habari, lini mtaanza kuandika habari zilizo kamilika? Kwa mfano; Huu mkopo una riba au lah? Unatakiwa kuanza kurudishwa lini na kwa kiasi gani? Serikali inatarajia kutoa wapi pesa za kulipia hili deni? Je kama tukishindwa kulipa, mkataba unasemaje? Kwa nini mkopo unapitia Exim bank ambayo nadhani ni benki binafsi? Nimechokaaaa na ninyi waandishi mpaka yani basi, maana vitu mnavyo andika siku hizi havina nukuu wala havielezi vilianzia wapi na wala vinaelekea wapi... Halafu grammar,spelling na sentence structure tuongelee siku nyingine... :)
ReplyDeleteKaka Michuzi hivi hawa waandaji wa hii bendera yetu kwa nini mara nyingi wanaiweka kichwa chini mihuu juu!!!!!!??????
ReplyDeletehapa kama riba itakuwepo hakika serikali itakuja kudaiwa zaidi ya billion 400,wakati mwingine naona ni bora kuvumilia shida tuliyokuwa nayo tukitafuta namna nyingine ya kuitatua kuliko kuchukua mkopo mkubwa kiasi hiki.
ReplyDeleteKabla ya yote hiyo bendera ya si tanzania kwani upande wa bluu huwa chini, labda kama una maana nji imepindiliwa.
ReplyDeleteJe wapi naweza pata kozi ya uwaziri wa fedha ili nitoe comments zenye mantiki.