Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Huyu baba yako peke yako kila mtu ana baba yake

    ReplyDelete
  2. Asante Ankal,umepata Kibali lakini??

    Huyo aliyetoa Comment ya kwanza,chukua IP address yake peleka "USHALAMA WA TAIFA",atafutwe.!

    David V

    ReplyDelete
  3. Wacha kutishia watu mshamba ww David V.
    Na mimi nasema huyu baba yako ww na huyo mleta post hii,nitafute na mm unipeleke unakotaka.

    ReplyDelete
  4. Hii ni karne ya 21, tujaribu kuheshima haki ya binadamu ya Kutoa maoni bila ya kutishwa. Mwalimu Nyerere anaheshimika duniani kote sio tu Tanzania, lakini pia siasa yake ilikuwa ina kasoro. Tumeshasahau kuwa hatukuruhusiwa kuwa na vyama vingi, kuwa na dola mfukoni, mistari ya kusubiri vyakula (resheni)na kadhalika. Kama tunataka heshima ndani na nje ya nchi, tuwe tayari kuheshimu haki za binadamu za kutamka bila ya vitisho vya kupeleka watu "Usalama wa Taifa". Mimi binafsi sio mpiga makofi wa siasa za Mwalimu na pili mali za wazazi zilichukuliwa na serikali kwa kuwa wazazi walifanya kazi kwa bidii bila ya kumwibia mtu wala serikali. Huu uchungu upo rohoni mwangu mpaka kufa. Anayepiga makofi ana haki ya kupiga makofi kwa Mwalimu lakini pia asiotaka kupiga makofi pia aheshimiwe kama tunataka kujiita nchi yenye haki za binadamu kwa wote.

    Ahsante Michuzi, nategemea utachapisha maoni yangu.

    ReplyDelete
  5. nadhani huyo aliecomment wa kwanza yeye si mmoja wa taifa letu.

    ReplyDelete
  6. This man was a genious tupende tusipende yaani aliona mbali sana na alichokisema ndio kinachotokea sasa. Wazanzibari wameshaanza kubagua watanganyika na ndani ya zanzibar pia wanabaguana wapemba na waunguja. Tutakukumbuka sana. May you continue to RIP!!

    ReplyDelete
  7. Ahsante anko mishuzi....
    Hiki kichwa ni noma....ananikosha kuanzia dk ya 24:49, na 25:43 na kuendelea kuhusu wazanzibari yaani wapemba na waunguja, anasema tunataka rais wa Tz na lazma atoke Zbr au Tanganyika (akijua Zbr ni waislam) iweje baadhi ya mazuzu leo waseme ni mdini na alitaka wakristo tu waongoze nchi?
    Anataka rais muislam au mkristu, hatujachagua asieamini Mungu ila akitokea ataapishwa kuilinda na kutetea katiba ya Tz.
    Kuhusu rushwa kanoga pia. Anaonekana alizungumza kwa vitendo pia, duh, alitandika wala rushwa viboko, mzee noma. Kuhusu serikali corrupt na wamachinga mtaani huku na kuanzia 58:30 JK ni muaminifu waliomzunguka je? kuanzia waziri mkuu aliejiuzuru na mawaziri waliotuhumiwa kwa rushwa nk. Huyu babu kama nabii vile wasiomkubali wabishi ila wanamsoma kimyakimya.
    Hotuba haichoshi mwanzo-mwisho, rekodi yake bado haijavunjwa.
    Maneno yake hayaendi bure tuombe uzima tutaona

    ReplyDelete
  8. bado wakimaliza kubaguana wazanzibar watajikuta wao ni wapemba na waunguja, na hakuna mpemba na muunguja watakuta kuna mmakunduchi, mburushi cjui, mkojani nk..Bado huo uenye heri anaopewa na Vatikan mnadhani bure?
    Ndo unabii wenyewe huu sio unabii koko wa akina fulani wanaokusanya sadaka za walalahoi makanisani.
    Michuzi umenipa munkari natzama hotuba zote za huyu babu hapa u tube, sina issue leo.
    Na leo naanza na hii ya 2 kushuka chini kulia aliomo Betty Mkwasa pembeni.
    Na ukiweza tafadhali tuwekeege japo kila siku ya kazi, wengine mpaka kazini kwenye net ya bure wkt wa mapumziko tujifunze toka kwake

    ReplyDelete
  9. kula tano mdau!! kama ulikuwepo hata mimi nimezikalia hotuba zake zote kuna moja anakemea udini kama alikuwepo ona mambo yalivyo sasa i tell you huyu tutamkumbuka daima continue to RIP.

    ReplyDelete
  10. Watanzania sisi wapole sana. Mwalimu Nyerere alilani rushwa, udini na kuwasaidia waafrika wengine kupigania uhuru wao. Lakini hapo hapo aliishikilia ncho kama kijiji chake, bila ya kutoa sauti kwa wanasiasa wengine. Haki za binadamu za kutoa maoni haikuruhusuwa na serikali ilikandamiza sauti za wananchi kama wakimpinga. Nchi ilienda katika umasikini haraka na bila ya China na Urusi, Watanzania wengi wangekufa na njaa vijijini. Ndio, tusimsahau Mwalimu Nyerere, lakini pia aliikandamiza nchi hii, naona watanzania wameshasahau njaa na vyakula kukosekana madukani, yote kwa sababu alikataa wafanyabiashara kuleta chakula kutoka nje au kutajirika kwa kuwa yeye ni Mjamaa, na kukandamizwa na serikali yake. Tumefika mbali sasa.

    ReplyDelete
  11. Mimi ni Mtanzania bara na nawaunga mkono Wazanzibari kama wanataka kutengana na Umoja wetu. Marais wa nchi hizi mbili hawajatupa sauti wanachi na kutuuliza kama tunataka umoja au la. Kama kawaida wakati wa miaka ya sitini, kulikuwa hamna utamaduni wa demokrasia na Marais wawili walitawala nchi zao kama vijiji vyao na wananchi waliopinga siasa zao walijikuta wako rumande bila haki zao kuheshimika.

    Kama tunaheshimu demokrasia, wananchi wa Tanganyika, Zanzibar na Pemba lazima wapewe sauti. Lazima waulizwe kama wanataka umoja au la, kwa kuwa hawakupewa sauti.

    Kuna nchi nyingi tu zilikuwa katika umoja lakini umoja wa kutumia nguvu na wananchi wao wakaamua wanataka kujitenga katika umoja huo kwa kutumia demokrasia ya kupiga referendum. Nchi hizi ni Czech na Slovakia. Singapore na Malaysia, Misri na Syria, na kadhalika. Mbingu hazijashuka na maisha yanaendelea kama kawaida kwa wananchi wao. Umefika muda kwa wananchi wa Tanganyika, Zanzibar na Pemba kupewa sauti zao na kuulizwa wazi katika referendum: Je, tunataka umoja au La? Tukifika hapo pasi tutajua kuwa demokrasia imekomaa. Hatujaulizwa kama tunataka umoja, sasa hivi demokrasia lazima iruhusu matakwa ya wananchi huru.

    Ahsante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...