Meneja wa masoko wa kampuni ya Kimataifa ya Data vision ltd  bibi Teddy Qirtu Ntemi akionyesha wandishi wa habari jinsi simu ya kiganjani inavyo weza kutafsiri lugha moja hadi nyigine kulia kwake ni mtafiti wa masoko bwana Patrick Minango na kushototo ni mtalamu wa kopyta bwana Emmanuel kagango uzinduzi huo ulifanyika makao makuu ya Data vision dar es salaam pcha na chris mfinanga

Kampuni ya Mobile Connect inayotoa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kutumia simu za mkononi wamezindua huduma mpya inayoitwa SMS Tafsiri.
 
Akizungumza katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Meneja wa Huduma hiyo, Bi. Teddy Qirtu alisema inalenga kusaidia watu wote ili wanufaike na simu zao za mkononi zaidi ya kuongea, kutuma ujumbe mfupi na kupata huduma za kibenki.
 
“Huduma hii ni ya kwanza kufanyika katika ukanda huu. Tumeianzisha kwa sababu tunaamini watu wengi wanapata changamoto ya kutaka kujua tafsiri ya neno au maneno katika nyakati tofauti kwa mfano wakati wa maongezi, katika kujaza fomu mbalimbali au kuandika barua”, alisema.
 
Alisema huduma ya SMS Tafsiri inayotumia lugha 15, inalenga kutoa ufumbuzi wa haraka, wakati wowote na mahali popote juu ya changamoto hizi kwa jamii. “Hivi sasa huduma ya SMS Tafsiri inatumia Kiswahili, Kiingereza, Kiarabu, Kichina, Kijerumani, Kifaransa, Kihindi, Kijapani, Kilatino, Kihispania, Kirusi, Kituruki, Kiebrania, Kiitaliano na Kiswidi,” alisema Bi. Qirtu.
 
Akifafanua kuhusu matumizi ya huduma hiyo, Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta wa kampuni hiyo, Bw. Emmanuel Kagongo alisema huduma ya SMS Tafsiri ina sehemu kuu tatu ambazo zinamuwezesha mtumiaji wa simu kutafsiri neno (word), kutafsiri sentensi (phrase) na kutambua lugha iliyotumika katika maandishi.
 
Akitoa mfano wa namna ya kutumia huduma hiyo, alisema mtumiaji anapaswa kutuma ujumbe mfupi wenye neno ‘tafsiri’ au ‘translate’ kwenda namba 15564 kwa kufuata maelekezo yaliyoainishwa.
 
“Kwa mfano, ili kutafsiri neno: Andika ujumbe ukiwa na neno la kwanza “Tafsiri” au “Translate”, acha nafasi, andika neno unalotaka kutafsiri, weka alama ya mkato, andika lugha ya kwanza, weka alama ya mkato, andika lugha unayotaka kutafsiriwa. Kisha tuma ujumbe wako kwenda namba 15564, na utapata maana ya ulichouliza kupitia SMS,” alisema.
 
”Ili kutafsiri sentensi, Bw. Kagongo alisema: unaandika ujumbe mfupi ukiwa na neno la kwanza “Tafsiri” au “Translate”, acha nafasi, andika sentensi unayotaka kutafsiri, weka alama ya mkato, andika lugha ya kwanza, weka alama ya mkato, andika lugha unayotaka kutafsiriwa. Kisha tuma ujumbe kwenda namba 15564.
 
Alisema taarifa zaidi za huduma hiyo zinapatikana kwenye tovuti ya www.mconnect.co.tz na kwamba kila ujumbe utatozwa sh. 250/-.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi mshasikia kitu kinaitwa google?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...