Ankal asalam aleikhum...
Nakutumia hii kukueleza maswahiba yaliyonikumba juzi katika hoteli ijulikanayo kama Aqua Lodge mjini Singida. Ni kwamba, baada ya kukodi chumba na kulala humo usiku, nilipokuwa naamka asubuhi na mapema ili kwenda kujenga taifa, nikastukia chaga ya kitanda inadumbukia chini kwa kishindo, na kwa bahati nilikuwa nimeshajiandaa kushuka kitandani. Na niliposimama pembeni mara besela linalobeba chandarua nalo likachomoka na kuangukia kitandani hapo puuuh!. Yaani haya yangetokea nikiwa nimelala kitandani hakika ningedhurika. Ama ningekuwa na mgombea mwenza hapo kitandani usiku sijui ingekuwaje...

Bosi wa hoteli hiyo hakuwepo wakati naondoka maana nilitaka nimkanye kwamba vifaa vibovu katika hoteli yenye hadhi kama hiyo vitakuja kumponza siku moja. Mfano mimi ningeumia hapo nisingekubali. Lazima tungefikishana mbali. Na hii si kwa hoteli hiyo pekee bali hoteli nyingi nyingine ambazo huduma zake na kastama kea huwa za magumashi wajitahidi hali kama hii na zingizne mbovu zisijitokeze.

Mdau Oljoro



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hivyo vitanda vya gesti kuna watu walikua wakiviita 'Wembley' sasa sijui wana na maana gani!!

    ReplyDelete
  2. Labda shughuli ilikuwa nzito.

    ReplyDelete
  3. "Wembley" yaani uwanja wa mpira wa ligi na mechi za kimataifa.Vitanda hivyo vyaitwa wembley kwa sababu ya mechi za mipira zinazochezwa hapo.You know what I mean.

    ReplyDelete
  4. Kuna jamaa aliyeangukiwa na dari katika chumba cha gesti moja, mwenye gesti akamwambia ni kwa sababu alikuwa anakoroma too much.

    ReplyDelete
  5. Kuna guest moja, ni kama guest bubu vile, iko jirani na baa. Majina ya vyumba vyake ni Amahoro, Old Traford, nk. Yaani ni majina ya viwanja vya mpira wa miguu. Mgeni akifika peke yake, anaulizwa mwenzako akifika tumruhusu aje au utakuja kumpokea mwenyewe? Ukisema kuwa upo peke yako unashangawa. Kwa ufupi ile ni GUEST ya watu kwenda KUBINJUKA!

    ReplyDelete
  6. hivi tutakuamini vipi kama si wewe ulikuwa na mechi Wembley?

    Pole Lakini

    ReplyDelete
  7. Ahhhh,

    Mdau wa Oljoro,

    Acha kuchinja kenge bila ganzi!

    Usitudangenye chaga za kitanda kwa hadhi ya Hoteli hiyo zilikuwa kamili isipokuwa ulikuwa na Mgombea mwenza na shughuli ilikuwa nzito sana ila yeye aliwahi kuondoka !

    Hapo Singida bana, wanajulikana wana mama mawejaza makalio sio mchezo !!!, kitanda ni wazi kilielemewa ukizingatia uzito huo na mshike mshike wa Lizombe usiku kucha unategemea tena chaga zisivunjike?

    Wewe chaga za mti mvule zitavunjika kirahisi?

    ReplyDelete
  8. Haiwezekani chaga zishuke bila shughuli pevu!!!

    ReplyDelete
  9. Mwanawame wa Oljoro,

    Kitanda hakiwezi kuvunjika kirahisi,

    Usiogope mambo nyumbani kwako kuharibika,

    Ni wazi ulipokuwa safarini Kikazi Singida ulikesha ukipiga (pu,,,m3u)

    ReplyDelete
  10. ahahahah....Pole sana kaka, unanikumbusha jamaa yangu mmoja guest zote maeneo ya Buguruni walikuwa hawamtaki..maana alikuwa vunja vitanda kila akiingia kwenye mechi.
    Ila kaka nahisi kulikuwa na tukio hapo usiku uliopita..Chaga, Chandarua vyote vianguke tu..Mhhh otherwise iwe Hadithi ya abunuasi.

    Umetisha.. Shemeji amekusamehe wewe tuelezee tu ilikuwaje?

    ReplyDelete
  11. Ahhh Mdau wa Oljoro ni wazi ulipokuwa safarini Singida kikazi ulikuwa unaosha jando!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...