Ankal asalam aleikhum...
Nakutumia hii kukueleza maswahiba yaliyonikumba juzi katika hoteli ijulikanayo kama Aqua Lodge mjini Singida. Ni kwamba, baada ya kukodi chumba na kulala humo usiku, nilipokuwa naamka asubuhi na mapema ili kwenda kujenga taifa, nikastukia chaga ya kitanda inadumbukia chini kwa kishindo, na kwa bahati nilikuwa nimeshajiandaa kushuka kitandani. Na niliposimama pembeni mara besela linalobeba chandarua nalo likachomoka na kuangukia kitandani hapo puuuh!. Yaani haya yangetokea nikiwa nimelala kitandani hakika ningedhurika. Ama ningekuwa na mgombea mwenza hapo kitandani usiku sijui ingekuwaje...
Bosi wa hoteli hiyo hakuwepo wakati naondoka maana nilitaka nimkanye kwamba vifaa vibovu katika hoteli yenye hadhi kama hiyo vitakuja kumponza siku moja. Mfano mimi ningeumia hapo nisingekubali. Lazima tungefikishana mbali. Na hii si kwa hoteli hiyo pekee bali hoteli nyingi nyingine ambazo huduma zake na kastama kea huwa za magumashi wajitahidi hali kama hii na zingizne mbovu zisijitokeze.
Mdau Oljoro

Hivyo vitanda vya gesti kuna watu walikua wakiviita 'Wembley' sasa sijui wana na maana gani!!
ReplyDeleteLabda shughuli ilikuwa nzito.
ReplyDelete"Wembley" yaani uwanja wa mpira wa ligi na mechi za kimataifa.Vitanda hivyo vyaitwa wembley kwa sababu ya mechi za mipira zinazochezwa hapo.You know what I mean.
ReplyDeleteKuna jamaa aliyeangukiwa na dari katika chumba cha gesti moja, mwenye gesti akamwambia ni kwa sababu alikuwa anakoroma too much.
ReplyDeleteKuna guest moja, ni kama guest bubu vile, iko jirani na baa. Majina ya vyumba vyake ni Amahoro, Old Traford, nk. Yaani ni majina ya viwanja vya mpira wa miguu. Mgeni akifika peke yake, anaulizwa mwenzako akifika tumruhusu aje au utakuja kumpokea mwenyewe? Ukisema kuwa upo peke yako unashangawa. Kwa ufupi ile ni GUEST ya watu kwenda KUBINJUKA!
ReplyDeletehivi tutakuamini vipi kama si wewe ulikuwa na mechi Wembley?
ReplyDeletePole Lakini
Ahhhh,
ReplyDeleteMdau wa Oljoro,
Acha kuchinja kenge bila ganzi!
Usitudangenye chaga za kitanda kwa hadhi ya Hoteli hiyo zilikuwa kamili isipokuwa ulikuwa na Mgombea mwenza na shughuli ilikuwa nzito sana ila yeye aliwahi kuondoka !
Hapo Singida bana, wanajulikana wana mama mawejaza makalio sio mchezo !!!, kitanda ni wazi kilielemewa ukizingatia uzito huo na mshike mshike wa Lizombe usiku kucha unategemea tena chaga zisivunjike?
Wewe chaga za mti mvule zitavunjika kirahisi?
Haiwezekani chaga zishuke bila shughuli pevu!!!
ReplyDeleteMwanawame wa Oljoro,
ReplyDeleteKitanda hakiwezi kuvunjika kirahisi,
Usiogope mambo nyumbani kwako kuharibika,
Ni wazi ulipokuwa safarini Kikazi Singida ulikesha ukipiga (pu,,,m3u)
ahahahah....Pole sana kaka, unanikumbusha jamaa yangu mmoja guest zote maeneo ya Buguruni walikuwa hawamtaki..maana alikuwa vunja vitanda kila akiingia kwenye mechi.
ReplyDeleteIla kaka nahisi kulikuwa na tukio hapo usiku uliopita..Chaga, Chandarua vyote vianguke tu..Mhhh otherwise iwe Hadithi ya abunuasi.
Umetisha.. Shemeji amekusamehe wewe tuelezee tu ilikuwaje?
Ahhh Mdau wa Oljoro ni wazi ulipokuwa safarini Singida kikazi ulikuwa unaosha jando!
ReplyDelete