Sekta ya gesi na mafuta ni moja kati ya sekta kubwa na ngeni kwa kiasi fulani hapa nchini.
Kwa kipindi cha miaka mingi na haswa miaka ya sabini na themanini Serikali ya awamu ya kwanza ilifanya kazi kubwa ya uwekezaji katika utafiti wa mafuta na gesi nchini  lakini bila ya mafanikio ya uwekezaji.
Hii inaweza kuwa ilichangiwa sana na siasa zilizokuwapo kwa wakati ule kwa maana ya umagharibi na umashariki na pengine imani ya wawekezaji kutokana na msimamo tuliokuwa nao kama nchi  katika suala la ukombozi wa bara la afrika dhidi ya ukoloni pia uduni wa hali ya teknologia ya wakati ule na ukweli kwamba eneo letu la nchi za mashariki mwa Afrika ilijulikana kuwa ni ukanda wa gesi asilia tu  na enzi zile gesi asilia ilikuwa haina thamani kuliko mafuta.
Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni , nchi yetu imefanikiwa sana kuwavuta wawekezaji katika sekta na nyanja tofauti  sana ikiwamo katika gesi na utafiti wa mafuta. Hii ni nafasi nzuri tuliyoikosa kwa miaka mingi kiasi cha kutuweka nyuma kimaendeleo ukilinganisha na nchi nyingi za afrika na dunia ya tatu.
Lakini sasa kiasi kikubwa tumeanza kuona manufaa ya uwekezaji ule japo kwa uchache na changamoto nyingi ndani yake.
Tumeanza mwaka 2012 na kumaliza na mfululizo wa matukio ya aina tofauti kwa waandishi kuandika makala na habari nyingi kuhusu shughuli na sekta nzima ya gesi nchini ,na mara ya mwisho kabisa kufuatia maandamano ya wanachi wa Mtwara ambao walitokea katika vyama  tofauti.
Sikuona tatizo la waandamanaji wale pamoja na ujumbe ulitolewa bali baadhi ya ujumbe  unaonyesha zipo tafsiri nyingi zaidi ya madai ya mahitajio ya manufaa ya mapato katika uwekezaji wa gesi na bomba la gesi.
Nilipata wasisiwasi mkubwa sana baada ya kuona wanaojua ukweli wa jinsi mambo yalivyo na wale wasiojua kuamua kwa dhati kabisa kuupotosha umma wa watanzania  na dunia kwa ujumla.

Murtaza Mangungu(MB)
Kilwa Kaskazini na mjumbe wa POAC


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Maandamano ni sawa, serikali zote hazijawahi kushughulikia matatizo ya kusini. Mfano, Kungekuwa na barabara na reli toka Mtwara hadi Songea, bidhaa zote za Malawi, Zambia na Kongo zingepita huko na kupunguza mzigo kwa bandari ya Dar na foleni zisizo za lazima. Kusema Dar yenye watu 4m inachangia 80% ya pato la taifa lenye watu 45m sio kitu cha kuvjivunia, inaonyesha jinsi gani uchumi wetu usivyokuwa balanced. Dar haina raslimali hata moja ya maana, ni ufisadi na ujanja ujanja tu.

    Hivi kweli inaingia akilini kujenga bandari mpya Bagamoyo! wakati Dar ipo? Si kuongeza ufisadi na msongamano usiokuwa wa lazima.

    Hivi waziri tena profesa anatoa mfano wa Mto Ruvu? Je maji utayazuia yasitiririke? Pata la mkazi wa Dar ni karibu 1m wa Mtwara ama Lindi ni kama 350,000/= Usawa hapo uko wapi halafu mnatuletea hadithi za abunuasi.

    Serikali inapaswa kubalance maendeleo kwa mikoa yote, Dar kuna vyou vikuu vya serikali karibu 10, je kwa nini Mtwara TTC haikupandiswa kuwa chuo kukuu badala yake ikawa Chang'ombe? Hiki ndicho watu wanaandamana.

    Lindi na Mtwara ni maskini wa kutupwa, gesi ilipofika wakaona ni sehemu ya wao kutokea kama Minofu (Mwanza), Kahawa (Moshi), utalii (ARUSHA) NK.

    Jameni tuweni na huruma, tunataka wamakonde waendelee kuwa walinzi?

    ReplyDelete
  2. Nashindwa kumuelewa huyo waziri aliyesema kuwa Mtwara kuna 14% tu ya gesi, Sasa kwanini wanajenga hilo bomba kwa gharama ya zaidi ya shilingi trilion moja nukta mbili za mkopo ambazo tunapaswa tuzilipe? Kama kiasi cha gesi ni kidogo na serikali inajua itakwisha muda si mrefu kama alivyodai waziri, sasa kwa nini bomba la kupeleka gesi Dar lijengwe? Kama ni hivyo basi serikali imekurupuka tu.

    ReplyDelete
  3. Sioni kwa nini huyu mbunge haelewi kwamba kusini kumesahaulika muda mrefu. Inaonekana ni mtu optimistic tu na watu wa huko kusini wamekuwa optimistic kwa muda mrefu na haijawasaidia. Kitu tunachoweza watanzania ni kuelezea matatizo, takwimu na kupeana moyo lakini kusini wako miaka mingi nyuma kulinganisha na mikoa mingine

    ReplyDelete
  4. Nahisi mheshimiwa anataka asikatwe jina lake kwenye uchaguzi ujao. Barabara toka uhuru mpaka leo haijakamilika wakati sehemu nyingine zinapanuliwa na zimekarabatiwa zaidi ya mara kadhaa. Wenyeji wanataka wahakikishiwe manufaa ya moja kwa moja na sio kama anayosema mheshimiwa.

    ReplyDelete
  5. Wamakonde wana haki! Shinyanga ni maskini kutupwa! Lakini dhahabu na almasi zatoka huko! Wamakonde wamejifunza kutoka kwa wasukuma! Big up kondez, mwendo ni uleule kwa kusonga mbele halafa wachichubutu kuchema, nchale hauna nguvu siku hizi, ila maandamano yana nguvu!

    ReplyDelete
  6. mradi huu wa gesi ni muhimu zaidi kwa Mtwara na lindi kuliko kwa Dar,
    upatikanaji wa urahisi wa nishati hii ya umeme kutaharakisha maendeleo ya mtwara kwa kasia ambacho haitarajiki,uwepo wa umeme kutaongeza kasi ya ujenzi wa viwanda zaidi ya cha cement,mbolea,plastic twaweza kupata pia viwanda vya kusindika matunda...matunda hayana mwenyewe pande hizi,kusindika samaki,bidhaa za ngozi n.k kwa hili kutaharakisha na kuongeza matumizi ya bandari kubwa kuliko zote tanzania ambayo haihitaji meli zikae foleni ili ziweze kufunga gati bandarini kwa kipindi cha miezi miwili hadi tatu kama ilivyo bandari ya dar!!!
    upatikanaji wa nishati hii mikoa ya mtwara na lindi kutaharakisha pia shughuli za utalii...unashangaa,hujui kuwa hifadhi ya wanyama kubwa kuliko zote ulimwenguni wka asilimia 80% imelala katika mikoa hii..tatizo la upatikanaji kirahisi la umeme na miondombinu mibovu kunafanya wageni watue Dar halafu kama ni kwa gari wasafiri mpaka Iringa ili waingie mbugani zaidi ya masaa 8 mpaka 9 wakati wakitumia gari kupitia lindi si zaidi ya masaa 5!!ukosufe wa miundombinu na umeme kumefanya kuwe hakuna mahoteli ya maana kupitia mlango huu wa rufiji,lindi na mtwara
    jambo lingine kuna mradi wa south corridor kwa mizigo ya Congo,Zambia na Malawi itakuwa rahisi kupitia Mtwara kuliko dar kwa ukaribu na ukubwa wa bandari yenyewe meli hazitakaa foleni kama dar na kuongeza ughali wa bidhaa bila sababu....na hili ni katika mambo yanayosababisha miradi hii isitekelezeke kwa kuwa mafisadi wengi wamewekeza dar..tutawaua kwa njaa huduma hizi za kibandari zikihamia mtwara..
    kingine kilimo unajua kwamba tuna bandari pale lindi ambayo ilikuwa inahusika na kusafirisha bidhaa za kilimo na mbaotuu!! mazao kama uele,chooko,mbaazi,korosho,mtama nk mikoa hii ilikuwa ikiongoza katika ukanda huu kuuza bara hindi kipindi hicho!!!??
    mikoa hii haihitaji pesa za serikali kuu kujengeka kama dar inahitaji uzalendo na sera zenye kutekelezeka inarasilimali nyingi kuliko dar ..
    ikiwa tutataka kuuza gas nje bandari ile ni kubwa mno kwa meli za ukubwa sana ambazo dar ni ndoto kuweza kufunga na tukitaka kuuza umeme nje mtwara inapakana na nchi nyingi itakuwa rahisi tu si kwambii urahisi wa kusafirisha umeme kulinganisha na kujenga bomba kwani hapa pana nini jamani tuwe wa kweli
    wanasema "the right is taken not given"umuhimu wa somo la historia kama mnaujua mtasikiliza wananchi wanataka nini kwani palisemwa...kule nchini poland "hapana jeshi lolote duniani lenye nguvu kushinda jeshi la wananchi" si maanishi JWTZ

    ReplyDelete
  7. huyu mbunge sijamwelewa kabisa anachokiongelea hapa. nahisi anaogopa kupoteza ubunge wake (kula). anatakiwa kujibu ni kwa nini kila kitu kiwe Dar. nikipata jibu safi mimi sina shida. ninachoelewa ni kwamba mafisadi hawawezi kuishi Mtwara au lindi na ili waendelee kufisadi wanataka kila kitu kiwe karibu nao. endeleza hata mikoa mingine.

    masuala mengine ambayo amesema; mimi nimepata wasi wasi na huyu mbunge kwani sijui kama anajua kazi yake vyema. mfano: amefanya juhudi gani kushawishi watu wasome veta, au amedhamini wangapi au ametafutia wangapi ufadhili kama mbunge (yaani kiongozi). kilimo, biashara n.k kafanya nini kuhakikisha nao wanafaidika. kila kitu kikiwa dar watawauzia nani maandazi, nyanya n.k. sidhani kama ni sahihikabisa kuchimba tanzanite ikawanufaisha watu wa Afrika kusini au kenya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...