Mwili wa mtoto huyo ukichukuliwa na polisi kwenda kuhifahiwa na kuchunguza chanzo cha moto huo
Nyumba hii ndimo alimoungulia mtoto huyo

Baadhi ya majirani wakiwa katika tukio hilo

Na Ezekiel Kamanga,Mbeya
Mtoto Halaika Bushiri (7) mwanafunzi wa shule ya msingi Mwanyanje iliyopo kata ya Igawilo jijini hapa amefariki dunia baada ya kuketea kwa moto akiwa nyumbani kwao jana majira ya saa 7:45 ya mchana, Januari 21 mwaka huu.

Shuhuda wa tukio hilo Recho Jeseph (36) amesema mtoto huyo aliza kupiga kelele za kuomba msaada mara baada ya kutokea kwa moto wakati mama wa mtoto Nuru Mlele akiendelea shughuli zake licha ya majira kujitokeza na kuuzima moto huo.
Katika hali ya kushangaza mama huyo hakuonesha kustushwa na kitu chochote na wakati tukio hilo aliendelea kufua nguo, hadi pale majirani walipofanikiwa kuudhibiti moto huo ambao uliteketeza samani za nyumba yake ikiwemo seti moja ya kochi na.


Aidha kutokana na juhudi za majirani kushirikiana ndani ya dakika kumi walifanikiwa kuudhibiti moto huo na kuuzima lakini mtoto huyo alikuwa tayari ameshafariki.

Hata hivyo licha ya polisi kupewa taarifa majira ya saa tisa kamiliwalifika majira ya saa kumbi na mbili na robo jioni, eneo la tukio lenye umbali wa mita mia sita kutoka kituoni, hali iliyowasononesha sana wananchi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa na uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. POLENI SANA WANA FAMILIA MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMEEN

    TUNAOMBA SERIKALI IJITAHIDI KUIMARISHA USALAMA WA RAIA KWA KUWEZA ULINZI WA HALI YA JUU WA KUPAMBANA NA WEZI MAJAMBAZI

    TUNAPOPATA WAGENI MBALI MBALI KUTOKA NJE YA NCHI HUWA WANATUPA MASWALI MENGI KUHUSIANA NA NYUMBA ZETU KUJENGEWA MACHUMA MILANGONI NA MADIRISHANI WENGI WA WAGENI HAO HUFIKIRI NI JELA BARIDI

    TANZANIA TUNAISHI KWENYE NYUMBA ZETU BILA AMANI WA FURAHA MTU HUWEZI KUJENGA NYUMBA BILA KUWEKA MACHUMA MILANGONI NA MADIRISHANI

    TUNAJIJENGEA JELA KWENYE NYUMBA ZETU KUTOKANA NA KUOGOPA WEZI MAJAMBAZI

    MFANO KUNAPOTOKEA MOTO KWENYE MIJENGO YETU NI HATARI SANA KWA MAISHA MAANA NAFASI YA KUKIMBILIA ITABAKIA MLANGONI PEKEYAKE MTU HUWEZI KUOKOA MAISHA KWA KUTOA DIRISHANI

    SERIKALI TUPENI AMANI WATANZANIA KWANI NGUVU UWEZO WOTE UPO KWENU WAKUU WETU.

    ReplyDelete
  2. Ukuta umeanguka na kuharibu magari, maafisi tele wa jeshi wa vyeo mbali mbali walifika kwa haraka sehemu ya tokeo, leo mtoto amefariki katika ajali ya moto na katika hali ya kutataniza maafisa wa jeshi wamechukuwa zaidi ya masaa matatu.

    Ama kweli masikini hana chake Tanzania!!!!!

    Lala pema peponi mtoto Halaika.

    ReplyDelete
  3. Mangi mkuu wa KiboshoJanuary 23, 2013

    Au ule uchawi wa Mbeya umerudi tena? Wanyakyusa wanaongoza kwa madhehebu mengi ya dini na wanaongoza pia kwa mambo ya USHIRIKINA!

    ReplyDelete
  4. Sleep tight little Angel, bongoland life is still cheap, the poorer you are, the cheaper your life is, so very sad!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...