Mkazi wa Kimanzichana Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Rajabu Juma Mkumba, akimuuliza maswali mbunge wa jimbo hilo Adam Malima (hayupo pichani) kuhusu kulipishwa mchango wa Shilingi elfu Ishirini ili kumuanzisha shule mtoto wa darasa la kwanza. Huku wakimtupia lawama mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kimanzichana kusini. Ambapo pia alimpa taarifa mbunge huyo kuwa wanawapeleka watotowao madrassa kwasababu adayao ni ndogo ukilinganisha na shule hiyo.
Mzee Said Hemedi Lihaku akimuuliza maswali Mbunge wa mkuranga kuhusu matibabu ya bure kwa wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 60 kuwa wanaambiwa ni bure lakini mbona wanalipishwa wanapokwenda hospitali.
Wakazi wa Kimanzichana wakifurahi wakati mbunge wao alipokuwa akiulizwa maswali ya kumuudhi na na kusababisha kuzungumza kwa ukali kwenye mkutano huo.

KATIKA  hali isiyo ya kawaida mkazi mmoja wa kijiji cha Kimanzichana Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Rajabu Juma Mkumba, amesema wananchi wa kijiji hicho wameacha kuwapeleka shule watoto wao na badalayake wanawapeleka  madrasa kutokana na gharama za madrassa hizo kuwa za bei ya chini kuliko Shule.
Akimuuliza swali mbunge wa jimbo hilo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Adam Malima, alisema wanashangazwa na kitendo wanachofanyiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kimanzichana Kusini cha kuwalipisha ada ya Shilingi Ishirini Elfu kwa motto mmoja anaetaka kuanza darasa la kwanza.
“Mheshimiwa mbunge Mkuu huyu wa shule anatoa wapi sharia ya kutuchangisha shilingi elfu ishirini (20,000) kwa kila mwanafunzi anaeanza darasa la kwanza? Wakazi wa hapa wengi wanaona bora watotowao wawapeleke madrassa kule kwasababu adayake ni ndogo,” Alihoji Mkumba.   
Lakini katika hali ya kushangaza mbunge huyo aligeuka mbogo na kuanza kuwafokea wananchi hao na kuwaambia hayo wamejitakia wenyewe kutokana na kutofanya juhudi ya kujenga shule nyingine kwani alishawaambia miaka miwili iliyopita kuwa watafute kiwanja ili ijengwe shule kwakua wao wanaongezeka sana.
“Nakumbuka miaka miwili iliyopita niliwaambia kwenye mkutano hapahapa kwamba kasi yetu ya kuongezeka  ni kubwa mno hivyo tujitahidi kutafuta kiwanja mapema ili tuwe na shule nyingine lakini hadi leohakuna kilichofanyika,” Alisema Malima.
Aidha mbunge huyo aliwaambia wananchi hao kama wanania ya kweli ya kutaka kutatua baadhi ya matatizo yao inawabidi wafanye ushirikiano wa dhati kwani wenzao wa kijiji Cha Mwalusembe walishirikiana nay eye wakaweza kujenga madarasa manne kwa siku 45 lakini kijiji hicho kinamiaka miwili hakijajenga hata darasa moja.
 
Mkutano huo ulikuwa ni wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa kujiunga kwenye mfuko wa afya ya jamii kwa wananchi kwenye Wilaya hiyo, ambapo wananchi wengi walionekana kuwa na maswali mengi yaliyokuwa nnje ya mada na maudhui ya mkutano huo hali iliyopandisha hasira za mbunge huyo na kuahidi atakwenda tena tarehe 17 mwezi huu kukutananao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. walikuchagua ili utafute viwanja vya shule zoote zitakazojengwa. si kazi ya wananchi bali yako wewe malima.

    ReplyDelete
  2. asante sana wananchi wa kimazichana kwanza aanze yeye mbunge kuwajibishwa kwa sababu hawaendi majimboni kwao kazi yao kukaa dar na kula pesa ya bure ya bunge si huyo mwalimu hana kosa mbunge asiwe mkali hafuatilii maswala ya wananchi wake asante wazee wa kimanzichana oyee

    ReplyDelete
  3. Kama yeye ni mbunge wao ni kwa nini yeye binafsi hashauri sehemu ya kujengwa shule mpya kijijini humo? kuwaambia wanakijiji watafute kiwanja sio sahihi kabisa. serikali kupitia kwake yeye mbunge ndio wanaotakiwa kutafuta kiwanja.

    ReplyDelete
  4. Wengi wetu sisi watanzania tunakosa sanaa ya kuongea na mabishano ( art of argument, persuasion and reasoning). Utakuta wengi wetu tuna paza sauti na kufokea tunapoongea hasa tukiwa tunatofautiana kifikra. Nimeona sana tatizo hilo hususan kwenye malumbano pale bungeni. Sio kila kitu tunaweza kujifunza kutoka kwa wazungu, lakini Hilo nahisi ni jambo jema kujifunza hasa ukiangalia jinsi wanavyo debate.
    Mdau,
    Mnama

    ReplyDelete
  5. Waache wananchi wamsulubu Mh. Mbunge wao, safi sana

    ReplyDelete
  6. Madrasa? swafi sana! kesho oh wakristo wanapendelewa!

    ReplyDelete
  7. nashukuru wananchi wa kimanzichana kwa kuamka.Heko wananchi wengine tuige mfano huo.

    ReplyDelete
  8. Pole sana Mheshimiwa. Unajimbo gumu sana,inaonekana uelewa wa watu ni mdogo sana na hata hao watoa hoja yaonekana wanatoka jimboni kwako. Hawana wanalojua! Wanakijiji wanapashwa kutoa eneo la ujenzi wa shule na si Mbunge. Mbunge na mhamasishaji asigeuzwe kuwa mradi. Tana katoa na mfano mzuri wa kijiji kingine ambacho tayari kwa uhamasishaji wake wameweza kushirikiana na Mbunge wao na kujenga madarasa 4. Sasa mtu mzima kama huyo anasema anampeleka mtoto madrasa badala ya shule ati madrasa ni rahisi, haya tuone hiyo ajira atakayopata baada ya kumaliza na kuhitimu madrasa. Mdau hapo sidhani kama wanamsulubu Mbunge wao kama uonavyo wewe, bali wanaonyesha ujinga wao na wanajisulubu wao wenyewe kwa maisha yao ya baadaye. Mheshimiwa usikate tamaa maeneo kama hayo ndio ya kutembelea mara kwa mara, wanahitaji msukumo zaidi kutokana na uelewa mdogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...