Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo majirani zake,Mzee Bernard Malyatabu Mayala (88) akiwa na mkewe Bi. Bernadetha Kabandime Msuluba (79) wakati alipowatembelea na kuwajualia hali na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2013 kijijini kwao Kibaoni Mkoani Katavi.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda anaonekana akiulizia bei ya nyama ya mbuzi wakati akiwa katika kijiji cha Kibaoni,Mkoani Katavi.Picha na Chris Mfinanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. maisha na kijijini yana raha zake

    ReplyDelete
  2. Hii ndiyo Likizo halisi...siyo kwenda dubai au south africa!!!

    ReplyDelete
  3. hahaha huyu jamaa anapenda sana life ya kijijini kwake. hata akipata holiday siku 1 anakwenda kwao maskini. safi sana PM

    ReplyDelete
  4. mmenikumbusha tu hivyo vidego (viti vya kukalia) ndo sababu wazee wetu hao wana migongo imara sio kama sisi tunaokalia masofas.

    ReplyDelete
  5. HUYU JAMAA 2015 IMEKA VIPI AU MPAKA AWE MTOTO WA TOWN WATANZANIA MSIMBANIE JAMAA ANA STAILI KUPEWA URAISI MAANA HANA LONGO LONGO SIO WENGINE MATANGAZO MARA KACHANGIA KANISA MARA KACHANGIA MISIKITI MARA ANAFANYA PATE YA KUFUNGA MWAKA HALAFU MBUGE MMOJA ANA MNADI MICHUZI IWEKE KAMA ILIVYO HII USI BANIE

    ReplyDelete
  6. The simplicity of scene is surely impressive and inviting, PM anaonekana mtu wa kuhenzi kwao. Safi sana

    ReplyDelete
  7. vigoda (viti vya kukalia) kaka inaonyesha uko Ulaya Miaka Mingi saana Mpaka Kiswahili kinakutoka
    Mdau
    25 Jan

    ReplyDelete
  8. Dr. Patrick NhigulaJanuary 07, 2013

    Dr. Patrick Nhigula,

    Ninafikiria hivi ni vizuri sana kwenda na kuongea na watu kusikiliza wanaongea nini. Kuishi miaka zaid ya 50 Afrika ni baraka sana.Ninafikiria serikali ya Tanzania waanzishe "Idara ya Wazee" itakayo angalia kutowa posho, matibabu, na huduma bure kwa wazee wa miaka 65 kwenda juu.

    ReplyDelete
  9. bomba sana.ingawa jamaa wanaonekana kumuogopa.Kiongozi ni kwa ajili ya watu sio misafara na ulinzi tight.

    ReplyDelete
  10. "Videgos" LOL, pengine wala si sababu ya kukaa ulaya muda mrefu. Inawezekana sana kwamba mdau ni "bongo fleva".Kiswahili cha "bongo fleva" kimepinda pinda tu.

    ReplyDelete
  11. Mtoto wa Mkulima !

    Very simple!

    Hana makuu anafarijika kutembea kwa miguu Kijijini kwao.

    Nafikiri hata hilo li VX V8 akishawasili nalo Kijijini kwao linakuwa limeegeshwa hadi siku yake ya kurudi Kazini!

    ReplyDelete
  12. Katika Kambarage Nyerere wachache tuliobakia nao kwa sasa ni huyu PM wetu!

    ReplyDelete
  13. Ni muhimu tukaendelea kuwa na Maraisi wasiopenda Makuu kama alivyo Mhe. Raisi JK na huyu Mzee mzima Mizengo Pinda!

    ReplyDelete
  14. Mizengo Pinda kama Kambarage Nyerere!!!

    ReplyDelete
  15. Safi sana Pinda ni mfano mzuri hata Cleopa Msuya nae alikuwa akipenda kula ckukuu nyumbani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...