Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi mkubwa wa mikutano wa Julius Nyerere multi-purpose International conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali. Picha na Freddy Maro.
Sehemu ya jukwaa kuu
Nafasi za wajumbe wa mikutano
Viti
Upande wa juu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. bwana maendeleo!!

    ReplyDelete
  2. UNAONEKANA NI UKUMBI MZURI SANA ILA PALE ULIPO SIJUI KAMA PARKING ITATOSHA? FANANISHA NA PARKING KAMA YA MLIMANI CITY HIVI

    ReplyDelete
  3. SAFI, DAR KULIKUWA HAKUNA UKUMBI WA MKUTANO. GARAMA ZA KUPELEKA MIKUTANO AICC ZITAPUNGUA

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa hatua iliyofikiwa kwa kupata Ukumbi mzuri!

    Nadhani ni wakati sasa wa kuachana na utaratibu wa Vikao vya kwenye Mabaa na Pubs kuendesha vikao nyeti huko.

    ReplyDelete
  5. UKUMBI UPO VIZURI JE?UPANDE WA PARKING ZA MAGARI N.K YAANI KWA UJUMLA TUONYESHWE PIA,TUNAOMBA MSAADA.
    mdau bwegenaz.

    ReplyDelete
  6. Ukumbi umesimama, mkandarasi ni nani? je ni mzawa? it's about time, wazalendo wapate hizi tenda, hata kama wajenzi na malighafi ni za wachina, sawa tu. Lakini mkandarasi mkuu awe mzawa, tafadhali.

    Michu, tafadhali tupatie jibu.

    Mdau NY.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...