Dear Uncle Michuzi,
niko safarini naelekea Tanga nikitokea Morogoro,Huku njiani najionea uendeshaji ambao ni hatari sana.
Naamini waweza kushawishi ushauri ufuatao kwa mabosi wa Jeshi la Polisi (upande wa Traffic Police).
Please, kama walivyotupatia simu za Viongozi wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya "ulinzi shirikishi" basi watupatie email address za makamanda wa mikoa wa traffic, ili tuwatumie hizi picha za ushahidi wa ukiukwaji mkubwa wa sheria za usalama barabarani.
Nakuhakikishia, hatua hiyo itapunguza makosa hayo na vifo vinavyosababishwa na uzembe wa madereva wetu.
Kila la kheri.
Mdau.
Kwa mie, hii line inawekwa pale ambapo kuna upungufu wa uonaji wa barabara huko mbele hivyo hairuhusiwi kumpita mwenzako. Mbaya zaidi ni hilo gari la nyuma, dereva wa basi anaweza chomoleza chap chap kwani anaona kijacho na kumwacha dereva afuataye katika majanga. Kuna nchi wanakubali kuwachukulia hatua madereva kwa picha na video. Sijui TZ ni vipi. Inasikitisha! Blackmpingo
ReplyDeletemsipoteze muda , hao polisi mtawapa mradi wa ulaji tu hakuna lolote
ReplyDeletebongo kuna vituko jamani, yaani hapo hata ilo basi alikustahili kulipita hilo lori kulingana na hiyo mistari juu ya barabara,, leseni za mezani hizi zinatumaliza kweli..
ReplyDeleteMPAKA WAWEKE NJIA MBILI MBILI TATIZO HILI KAMWE HALITAKWISHA.
ReplyDeletepicha si ushahidi makini kwani fotoshop inweza kutia hatia waso hatia.
ReplyDeleteKwani ushahidi wa picha za kielekitroniki unakubalika kwa mujibu wa sheria zetu?
ReplyDelete