Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo.Kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Yusuf Mwenda na mbunge wa Ubungo John Mnyika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo.Kushoto anayeangalia ni mbunge wa Ubungo John Mnyika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waishio eneo la Golani Kimara Suka muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani.
Wananchi wa vyama mbalimbali vya Siasa wakishangilia wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwahutubia muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam leo mchana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Madabida,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik Meck Sadik,Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda na kushoto ni Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika.
HA HAAA NAONA MAKADA, MAKAMANDA NA NGUNGURI WANAPIGANA VIKUMBO NA BENDERA ZAO KAZI KWELI KWELI...
ReplyDelete