Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mtoto wa Ughaibuni ni wa Ughaibuni tu, tena wazazi muachane na tabia za kutaka wajue Bongo. Diaspora waliofanikiwa mpaka sasa kudhibiti watoto wao ni Wapakistani pekee. Mpakistan akirudi tu kazi au shule yupo nyumbani, anajichanganya na Wapakistan wenzao tu, akifika umri wa kuoa au kuolewa anatafutiwa mchumba kwao Pakistani. Mpakistani anachojua yeye ni kazi au shule basi. Mpakistani hupo tayari kwenda jela kwa toto lake lisilofata maadili ya kwao. Watoto walioshindikana kwa wazazi wao wa Kipakistani wanalelewa na serikali za Ughaibuni au wamezikwa.

    Hapa UK watoto wenye malezi mabaya ni watoto wa watu wa kipato cha chini. Sasa hawa ndio wenye kuchanganyika na watoto wa wahamiaji. Hapa UK mashoga wanachekwa na kudharauliwa lakini sio sheria na serikali inawalinda. Uvaaji wa nguo zinazo onyesha sehemu za mwili kama Rihanna au Lady Gaga vile pia raia hapa hawapendi lakini serikali inawalinda wavaaji.

    ReplyDelete
  2. Hi! Kipindi chenu poa sana!! huwa nakifurahia sana hususani mahojiano yenu hasa nikizingatia hoja za bwana Benja Mwaipaja, Mdau huyu hunifurahisha sa na kucheka sana kwa hoja zake za kusema ukweli bilan kukopesha na hata mimi kama mtz niliyopüo hapa Europe nauunga sana hoja zake na ukweli wake ambao Mwipaja huwa anauongea. Ukweli sisi Wtz(Waafrika) huwa hatupendi mtu ambaye ni muwazi sana na mawazo yake na nafikiri bwana Mwaipaja anajaribu sana kutokomeza suala la kutokuambiana ukweli kiwziwazi na mawazo yake nayaunga mkono sana. Imefika wakati wa atz kuambiana anakwa ana ukweli bila kupitia mlango wa nyuma na hili nimeliona sana kwa bwana Mwaipaja katika vipindi vyote vilivyopeperushwa jinsi anvyotoa ukweli wa maisha na tabia msimamo wa hko Marekani, ndani ya wtz wenyewe walioko huko na waliopo Bongo. Bwana Mwipaja endeleza msimamo huo!!!!!na Bwana jongo asnte sana kwa kipindi chako kina changamoto kubwa sana ikiwezekana itapendeza zaidi ikiwa kipindi chako kingepanta nafasi kwenye ITV bongo ili Watz waelimishwa zaidi kimaisha sio darasani: Elimu ya maisha haiko darasani hata siku moja , maisha ni mtazamo wa mapambano na marumbano ya jamii,na nchi au mahali lipo na sio ulikozaliwa au ulipoishia darasani!! Nawatakia Waandalizi wote w kipndi hiki waendelee na moyo huu wa kuwaelimisha watu na pia nawatakia kila la heri kimaisha huko mlipo.
    Ni mimi mdau kutoka Germany
    Benos

    ReplyDelete
  3. aisee kaka mwenye t-shirt ya blue ngoja nikupongeze. Siku zote nilikuwa naona unapiga tu kelele kwenye hiki kipindi. Ila leo kaka umeongea maneno yenye akili sana, hongera na endelea hivyo.

    ReplyDelete
  4. nakubaliana na kaka Benja, mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo. ukipika chakula akikataa na wewe ukawa unafanya tu vitu anavyo taka mtoto badala ya kumfunza kwamba katika maisha huta pata siku zote kile unacho taka basi unamharibu.

    Lazima pawe na tofauti kati ya mzazi na mtoto, mtoto hawezi kumwendesha mzazi. sio lazima umchape mtoto kuna njia mbadala zaku muadhibisha, mfano hiyo ya wengine wanakula nyama wewe unakula kabichi mpaka ubadili tabia.

    ReplyDelete
  5. Mtoto mleavvyo ndivyo akuavyo!

    ReplyDelete
  6. Ushauri wa bure kipindi ni kizuri ila jaribuni kubadilisha Outfit ili tuweze kutofautisha kipindi cha leo na kilopita,ahsante.

    ReplyDelete
  7. Jamani tunayo 911 Tanzania ila kule kwetu ni 999.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...