Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid  akizindua wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati) akipokea mfano wa ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakati wa kukabidhi jengo la wodi ya watoto ya Hospitali ya Mkoa wa  Morogoro,  ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika mjini Morogoro juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey.
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati), akishiriki kufanya usafi katika jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki ya CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Dk. Charles Kimei akishiriki katika zoezi la kufanya usafi. Hafla hiyo ilifanyika mjini Morogoro juzi. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiteta jambo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Mashishanga.
 Jengo la Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ikionekana ikiwa katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati na Benki ya CRDB na kugharimu kiasi cha sh. milioni 50.
 Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo (kushoto) akifurahjia jambo na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kati) na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey. 
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa wameshika miche ya miti tayari kwa kuanza zoezi la upandaji miti kuzunguka katika maeneo ya hospitali ya Mkoa wa Morogoro. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Asante CRDB maana hilo jengo lilikua linatishia afya za watoto

    ReplyDelete
  2. AHSANTE SANA CRDB BANK, MWENYEZI MUNGU AWAWEZESHE ZAIDI. JAMAA WA UPANDE WA KULIA HATA HAJUI MAANA YA MICHE KAFUATA MKUMBO TU, UTASHIKAJE MCHE WENYEWE HUKU SEHEMU YA MIZIZI YENYE UDONGO IKINING'INIA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...