Kijiji cha Mkoka wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma kina mbwa wengi sana. Mmoja wao alikatisha katikati ya kadamnasi leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Shirika la Mfuko wa Changamoto za millenia (MCC) ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Mradi huo utanufaisha jumla ya vijiji 16 vya Dodoma kuwa na umeme wa uhakika
 Baada ya kuona mbwa huyo akielekea jukwaa kuu, Ras Makunja mmoja akajitokeza na kuzuia tafrani ambayo ingejitokeza endapo mbwa huyo angetinga jukwaa kuu...
Akionesha ukakakamavu wa hali ya juu Ras Makunja huyo aliweka mambo sawa kwa kumwelekeza mbwa huyo kwengineko. Ni tukio la sekunde tatu lakini Kamera ya Globu ya Jamii iliweza kurekodi kila hatua kama inavyoonekana....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. mwe !mwe ! mwe! Kikamanda ketu Ras Makunja a.k.a field marshal,mkuu wa anunnaki empire,naona akiwa kazini kwake

    ReplyDelete
  2. huyu mbwa anacheza kamanda ras makunja,atageuzwa kitowewo

    ReplyDelete
  3. chezea ! ras makunja ,huu muziki anaoutaka huyu mbwa ? angepigwa kabali za kikariakoo,

    ReplyDelete
  4. kamanda ras makunja hilo jibwa lingeleta za kuleta lingejikuta linachomwa mishikaki,mjengwa nyama hiyooo

    ReplyDelete
  5. kiasi cha mbwa kajua wapi? kwa kukimbilia vingevyo sebene lake lingekua kubwa,tunavyomjua kamanda ras makunja

    ReplyDelete
  6. hili jibwa linataka kuchezeshwa bongo tambabare ya ras makunja

    ReplyDelete
  7. sio mchezo mbwa anataka muziki wa Ras Makunja

    ReplyDelete
  8. duh! ras makunja huyu mnyama ungempata ungefuta uchache kutoka kina mjengwa na Galinoma aka butijiwe

    ReplyDelete
  9. mungu wangu kijibwa kimekatiza katika anga za kamanda ras makunja,

    ReplyDelete
  10. Field-marshal kamanda ras makunja naona huyo mbwa anataka muziki,sasa kamanda tuongee basi iko kigitaa kiunoni mie nimefika bei

    ReplyDelete
  11. Field-marshal kamanda ras makunja naona huyo mbwa anataka muziki,sasa kamanda tuongee basi iko kigitaa kiunoni mie nimefika bei

    ReplyDelete
  12. naona leo supu ya mawe itakua ya mbwa,ras makunja hapo mpaka kieleweke

    ReplyDelete
  13. eboo! hiki kijibwa kinataka kumfundisha kazi Ras makunja tena mbele ya amiri jeshi mkuu! Ras makunja vijibwa kama hivi achezi navyo hapa leo kingeeleweka kama kijibwa kingejaribu kubwaka

    ReplyDelete
  14. huyu mbwa kama asingefuata njia nyingine tunajua ras makunja lazima angeanza nae na sebene,usifanye mchezo na ras makunja mbele ya muzuki wake

    ReplyDelete
  15. te!te! mbwa anataka kuchafua hali ya hewa katika himaya ya Ras Makunja?
    mkuu ras makunja hataki kuona fujo fujo kama hizi tena mbele ya mkuu wa dola.mbwa si bure katumwa anataka kuvurunda kazi ya ras makunja,tena aliyemtuma mbwa huyu ashukuru hapa pana JK kama wangekua watu wengine tuu muziki ungeanza

    ReplyDelete
  16. hiiii! Ras makunja naona huyu bobi anataka kukuharibia kazi

    ReplyDelete
  17. wewe mbwa huna adabu? ukatize mbele ya ras makunja hata siku moja haiwezekani rudi ulikotumwa

    ReplyDelete
  18. ah ,ras makunja naona mbwa anataka kuloga kazi! anavamia hadi kwenye himaya yako? kaponea chupu chupu kama asingekuapo mkuu hapo najua ungemchezesha bongo tambarare

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...