Wanajeshi
wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC) wametakiwa kudumisha utamaduni wa
askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani kwa
kuifanya kazi hiyo kwa heshima, nidhamu na utii ili kulinda heshima yao wenyewe
na ile ya Tanzania.
Askari
hao wamekumbushwa utamaduni huo wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika
maeneo mbali mbali duniani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais
na Amiri Jeshi Mkuu alikuwa akiwaaga wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda
amani chini ya Umoja wa Mataifa katika DRC katika hafla iliyofanyika leo,
Jumatano, Mei 8, 2012, kwenye Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu la
Tanzania yaliyoko Msangani, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Akizungumza
na askari hao, Rais Kikwete amewaambia kuwa hana wasiwasi kuhusu uwezo wao wa
kutelekeza majukumu yao yanayowapeleka DRC isipokuwa tu kwamba waifanye kazi
hiyo vizuri na kulingana na utamaduni wa majeshi ya kulinda amani ya Tanzania
katika sehemu mbali mbali duniani.
“Tunakwenda
kutelekeza majukumu ya Umoja wa Mataifa, sina shaka kuwa majukumu yenu
mnayaelewa vizuri. Kazi yetu ni kulinda amani na wala hatuendi kupigana na yoyote.
Kazi ya kijeshi mnaijua vizuri vile vile na kwa hili pia sina wasiwasi hata
kidogo,” amesema Amiri Jeshi Mkuu na kuongeza:
“Kubwa
ambalo lazima tulikumbuke ni kwamba nchi yetu kila ilikopeleka majeshi ya
kulinda amani imejenga utamaduni wa pekee. Imejenga utamaduni wa askari wetu kuifanya
kazi ya kulinda amani kwa heshima, kwa nidhamu na kwa utii wa kiwango cha juu. Hii
ni heshima kwetu binafsi na heshima kwa taifa letu. Nawashukuruni na nawatakie
kila la heri”
Kama
ishara ya kuagana na askari hao, Rais na Amiri Jeshi Mkuu amemkabidhi Bendera
ya Taifa Luteni Kanali Orestess Cassian Komba, Kamanda wa Kikosi cha Tanzania
katika DRC ambacho kitajulikana kwa jina la TANZBATT 1-DRC, akimwambia “Bendera
na Ikapepee”.
Katika
jukumu la kulinda amani Mashariki mwa DRC, Kikosi cha Tanzania chenye askari
1281, kitajiunga na vikosi vya Malawi na Afrika Kusini ambavyo vyote vitakuwa
chini ya Kamanda wa Brigedi hiyo, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa wa
Tanzania pia. Kundi la kwanza la askari hao Tanzania linaondoka nchini kesho.
Majeshi
hayo ya Tanzania yatalinda amani katika DRC chini ya Azimio Nambari 2098 (2013)
la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
8 Mei, 2013
Tanzani bib up sana Mungu atawasaidi katika hali yote ngumu mtakayo kumbana nayo huko DRC jaribuni kuwaretea amani hao wakongo ambayo yameikosa kwa mda Mrefu.Msiogope hivyo vitisho vya M23 japo wana suport kutoka Nchi jirani.
ReplyDeleteHii inatia moyo mzee wetu Rais Kikwete.
ReplyDeleteNaomba na membomengine support kwa hali hivyo hivyo, na mengine yaliyopinda yatanyooka.
Mzee ajali za barabarani zimemaliza ndugu zetu. Wenye magari ni maafande wa viongozi uliowateua. madereve wamekuwa wajeuri kwa sabb wanaendesha magari ya wakubwa . Mzee liangalie hilo nalo. wape somo hao viongozi wawaadabishe, wawashauri madereva wao kama unavyofanya hapa pichani. Nchi itaenda vizuri sana.
Mzee usinyamze kuwategemea akina Kaga na wengine. Wanakuhabibia hawa. Wanaifanya ccm ichukiwe kinoma. Fungua mdomo ongea na hawa nchi yetu ni nzuri imeharibiwa
Nidhamu ni kitu chema sana. Tanzania ilikuwa na nidhamu kupindukia. Ilitegemewa na nchi nhingi barani Africa ktk kulinda amani. Lakini sasa ni kichekesho. Tunalinda amani ktk nchi za wenzetu huku kwetu mabomu kula kukicha.
ReplyDeleteNa hii hali inaonekana kulindwa na kuimarishwa.
Hebu toa tamko mzee sema SASA MABOMU BASI. tutaona atakayekohoa.
Mhe. Raisi JK,
ReplyDeleteVipi na yule mama kule Malawi?
Kwa nini nako kusitumwe Kikosi angalau kwa uchache Battalion moja ya Mgambo?
Moja kwa moja madai yake kuhusu umiliki wa Ziwa lote hayana msingi, hata Jumuiya ya Kimataifa inalifahamu hili kwa kuwa anaonekana kuzingatia sana SHERIA ZA MKOLONI wakati nchi sasa zipi huru na zinatumia Sheria za Kimataifa.
Mgambo peke yake watatosha kumshikisha adabu, kwa kuwa hatuna sababu ya kutumia vifaa vyetu ambavyo kwa Malawi vipo juu mno.
Ingefaa naye angetumiwa Majeshi akachapwa!
Hodi hodi M-23 !
ReplyDeleteWenyewe kjisalimishe kwenye Kambi za Wakimbizi Rwanda na Uganda kabla hamjatiwa mkononi.
Nimelipenda Hilo jukwaa walilomwandalia Mheshimiwa
ReplyDeleteTANZANIA kila siku ni Mshumaa na huu ndio utamaduni m-bovu sana uliowachwa na NYERERE
ReplyDeleteYeye badala kujali maendeleo ya Nchi akajihusisha na Amani za watu wengine na kutuwacha maskini
Vita au Hata kulinda Amani siku zote ni Gharama tena gharama kubwa ijapokuwa tuta argue kuwa UN ndio wanasaidia.
Nchi imejaa mabalaa hakuna hata moja linalotatuliwa mi KINANITIA SHAKA SANA kipindi hiki kila siku MARA TUMETEMBELEWA NA MAJESHI YA GHANA MARA NIGERIA MARA SOUTH AFRICA je tunajua nini hao wanakitafuta isiwe wanapima uwezo wetu maana tunawapeleka na vituo vya habari pia
WAPE wape neno baba. hawa wajeshi nao noma.Bora waende wapigane na wajeshi wenzao kama itatokea lakini hatuombei. Maana hapa TZ wanapigana hata na watoto wadogo sabb hawana kazi ya kufanya. Wanapigana na watoto bila hata kuwianisha nguvu na umri wao na watoto.
ReplyDeleteHapa kazi wameipata..Lakini binadamu ni binadamu..hawa ndio tunawategemea watulinde lakini nao lazima wapigwe msasa kabla ya kuondoka
SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA RAIS JAKAYA KIKWETE NA JESHI LA TANZANIA KWENDA DRCONGO KUUNGANA NA JESHI LA UMOJA WA MATAIFA KULINDA AMANI...
ReplyDeleteWATANZANIA NI WAKARIMU, WAPENDA AMANI.