Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya  wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na  jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,  katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013. 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
 Wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wametakiwa kudumisha utamaduni  wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani kwa kuifanya kazi hiyo kwa heshima, nidhamu na utii ili kulinda heshima yao wenyewe na ile ya Tanzania.
Askari hao wamekumbushwa utamaduni huo wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikuwa akiwaaga wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa katika DRC katika hafla iliyofanyika leo, Jumatano, Mei 8, 2012, kwenye Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu la Tanzania yaliyoko Msangani, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na askari hao, Rais Kikwete amewaambia kuwa hana wasiwasi kuhusu uwezo wao wa kutelekeza majukumu yao yanayowapeleka DRC isipokuwa tu kwamba waifanye kazi hiyo vizuri na kulingana na utamaduni wa majeshi ya kulinda amani ya Tanzania katika sehemu mbali mbali duniani.
“Tunakwenda kutelekeza majukumu ya Umoja wa Mataifa, sina shaka kuwa majukumu yenu mnayaelewa vizuri. Kazi yetu ni kulinda amani na wala hatuendi kupigana na yoyote. Kazi ya kijeshi mnaijua vizuri vile vile na kwa hili pia sina wasiwasi hata kidogo,” amesema Amiri Jeshi Mkuu na kuongeza:
“Kubwa ambalo lazima tulikumbuke ni kwamba nchi yetu kila ilikopeleka majeshi ya kulinda amani imejenga utamaduni wa pekee. Imejenga utamaduni wa askari wetu kuifanya kazi ya kulinda amani kwa heshima, kwa nidhamu na kwa utii wa kiwango cha juu. Hii ni heshima kwetu binafsi na heshima kwa taifa letu. Nawashukuruni na nawatakie kila la heri”
Kama ishara ya kuagana na askari hao, Rais na Amiri Jeshi Mkuu amemkabidhi Bendera ya Taifa Luteni Kanali Orestess Cassian Komba, Kamanda wa Kikosi cha Tanzania katika DRC ambacho kitajulikana kwa jina la TANZBATT 1-DRC, akimwambia “Bendera na Ikapepee”.
Katika jukumu la kulinda amani Mashariki mwa DRC, Kikosi cha Tanzania chenye askari 1281, kitajiunga na vikosi vya Malawi na Afrika Kusini ambavyo vyote vitakuwa chini ya Kamanda wa Brigedi hiyo, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa wa Tanzania pia. Kundi la kwanza la askari hao Tanzania linaondoka nchini kesho.
Majeshi hayo ya Tanzania yatalinda amani katika DRC chini ya Azimio Nambari 2098 (2013) la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Mei, 2013


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2013

    Tanzani bib up sana Mungu atawasaidi katika hali yote ngumu mtakayo kumbana nayo huko DRC jaribuni kuwaretea amani hao wakongo ambayo yameikosa kwa mda Mrefu.Msiogope hivyo vitisho vya M23 japo wana suport kutoka Nchi jirani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2013

    Hii inatia moyo mzee wetu Rais Kikwete.

    Naomba na membomengine support kwa hali hivyo hivyo, na mengine yaliyopinda yatanyooka.

    Mzee ajali za barabarani zimemaliza ndugu zetu. Wenye magari ni maafande wa viongozi uliowateua. madereve wamekuwa wajeuri kwa sabb wanaendesha magari ya wakubwa . Mzee liangalie hilo nalo. wape somo hao viongozi wawaadabishe, wawashauri madereva wao kama unavyofanya hapa pichani. Nchi itaenda vizuri sana.

    Mzee usinyamze kuwategemea akina Kaga na wengine. Wanakuhabibia hawa. Wanaifanya ccm ichukiwe kinoma. Fungua mdomo ongea na hawa nchi yetu ni nzuri imeharibiwa

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2013

    Nidhamu ni kitu chema sana. Tanzania ilikuwa na nidhamu kupindukia. Ilitegemewa na nchi nhingi barani Africa ktk kulinda amani. Lakini sasa ni kichekesho. Tunalinda amani ktk nchi za wenzetu huku kwetu mabomu kula kukicha.

    Na hii hali inaonekana kulindwa na kuimarishwa.
    Hebu toa tamko mzee sema SASA MABOMU BASI. tutaona atakayekohoa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 09, 2013

    Mhe. Raisi JK,

    Vipi na yule mama kule Malawi?
    Kwa nini nako kusitumwe Kikosi angalau kwa uchache Battalion moja ya Mgambo?

    Moja kwa moja madai yake kuhusu umiliki wa Ziwa lote hayana msingi, hata Jumuiya ya Kimataifa inalifahamu hili kwa kuwa anaonekana kuzingatia sana SHERIA ZA MKOLONI wakati nchi sasa zipi huru na zinatumia Sheria za Kimataifa.

    Mgambo peke yake watatosha kumshikisha adabu, kwa kuwa hatuna sababu ya kutumia vifaa vyetu ambavyo kwa Malawi vipo juu mno.

    Ingefaa naye angetumiwa Majeshi akachapwa!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 09, 2013

    Hodi hodi M-23 !

    Wenyewe kjisalimishe kwenye Kambi za Wakimbizi Rwanda na Uganda kabla hamjatiwa mkononi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 09, 2013

    Nimelipenda Hilo jukwaa walilomwandalia Mheshimiwa

    ReplyDelete
  7. TANZANIA kila siku ni Mshumaa na huu ndio utamaduni m-bovu sana uliowachwa na NYERERE
    Yeye badala kujali maendeleo ya Nchi akajihusisha na Amani za watu wengine na kutuwacha maskini

    Vita au Hata kulinda Amani siku zote ni Gharama tena gharama kubwa ijapokuwa tuta argue kuwa UN ndio wanasaidia.

    Nchi imejaa mabalaa hakuna hata moja linalotatuliwa mi KINANITIA SHAKA SANA kipindi hiki kila siku MARA TUMETEMBELEWA NA MAJESHI YA GHANA MARA NIGERIA MARA SOUTH AFRICA je tunajua nini hao wanakitafuta isiwe wanapima uwezo wetu maana tunawapeleka na vituo vya habari pia

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 09, 2013

    WAPE wape neno baba. hawa wajeshi nao noma.Bora waende wapigane na wajeshi wenzao kama itatokea lakini hatuombei. Maana hapa TZ wanapigana hata na watoto wadogo sabb hawana kazi ya kufanya. Wanapigana na watoto bila hata kuwianisha nguvu na umri wao na watoto.

    Hapa kazi wameipata..Lakini binadamu ni binadamu..hawa ndio tunawategemea watulinde lakini nao lazima wapigwe msasa kabla ya kuondoka

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 09, 2013

    SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA RAIS JAKAYA KIKWETE NA JESHI LA TANZANIA KWENDA DRCONGO KUUNGANA NA JESHI LA UMOJA WA MATAIFA KULINDA AMANI...
    WATANZANIA NI WAKARIMU, WAPENDA AMANI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...