Watu Nane wamefariki Dumia baada gari walilokuwa wakisafiria aina ya Isuzu lenye nambari za usajili T.677 ADL (lori) ,wakitoka Kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo Kwenda Songea kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Hanga eneo la Bombambili wilayani Namtumbo mkoa wa Ruvuma.

Lori hilo lilikuwa limebeba Roli magunia ya ufuta, mpunga wakiwemo na hao abiria

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma,Deusdedit Nsimeki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo ilitokea Jana Majira ya saa nne na nusu (4:30 usiku) katika Kijiji cha Hanga eneo la mkoa wa Ruvuma bombambili, Chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi wa dereva huku akiendesha akiwa amelewa.

Lori hilo ambalo ni Mali ya mfanyabiashara wa mazao,likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN Nyoni Mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI SONGEA, Baada ya ajali hiyo kutokea dereva wa Lori Hilo alikimbia na kutelekeza lori hilo porini hadi Sasa jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma linafanya jitihada za kumtafuta ili sheria ifuate mkondo wake.

Kamanda wa Polisi amesema,Lori hilo liliacha Njia baada ya kugonga daraja na kupinduka hali iliyopelekea vifo vya watu Nane (8) na wengine kumi na Moja (11) kujeruhiwa ambao Wote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    Michuzi tafadhali kabla ya kutuma au kuweka habari, ingekuwa vizuri ungezihakiki naona kila siku kuna utumiaji mbovu wa maneno ya kiswahili. mfano hapo juu kichwa cha habari kinavyosema watu nane wamefaliki na mmoja kujeluhiwa. usahihi ni kuwa watu nane wamefariki na mmoja kujeruhiwa. Michuzi kama si wewe uliyetuma habari hii basi inabidi uwajibishe hao wasaidizi wako. kwa maana makosa hayo yanaonekana kila wakati utakuja kuiharibu blog yako bure .
    ni mtazamo wangu tu.
    mdau wa Mahuta shimoni Mtwara.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2013

    Poleni kwa msiba.Jamani naomba tujitahidi kuandika lugha sahihi.Mwandishi unaandika Wafaliki dunia badala ya Wafariki.Tuwe makini na herufi ni sawa na wengi wetu tunakosea sana herufi mfano RAHA mtu anatamka LAHA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2013

    kalewa anaendesha gari; mbele anaona kiza. Ameua watu; adhabu yake nini huyu.... Nafikiri serikali idhibiti hii pombe kwa kuongeza kodi maradufu hadi bia moja iuzwe milioni moja. Hapo ajali zitapungua...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2013

    mkuu hizo L ziondoe na kuweka R.

    Kiswahili ndio lugha tunayoitaka basi tuitumie ipasavyo, isije ikaonekana hata chenyewe kinatupiga chenga.

    Wafiwa poleni

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2013

    Jamani jifunzeni kutumia R!!!! hakuna maneno kufaliki wala kujeluhiwa!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2013

    Michuzi!! Hao vijana wako wanakuangusha sana. Hii glob sasa hivi imeshakuwa na heshima ya kimataifa, makosa madogo madogo ya uzembe wa lugha namna hii hayawezi kustahamilika. Uzembe huu lazima ukome na ukome sasa.
    Tunaomba umuachishe kazi huyu mzembe asizidi kutuharibia glob yetu na tafuta mtu mwenye adabu yake anayeweza kufit.

    ReplyDelete
  7. Kwanza poleni nyote mliofikwa na ajali pamoja na msiba huo. Madereva pia inabidi muwe makini mnapokuwa kwenye 'usukani' japokuwa ajali haina kinga, lakini tujitahidi ili kunusuru maisha ya abiria wetu na mali zao.

    Hivi na haya makosa hayo katika utumiaji fasaha wa kiswahili yatakwisha lini? Maana imeshakuwa ni kama desturi sasa huku tukijisifia kuwa Kiswahili ndio lugha ya Taifa letu, wakati baadhi yetu hata ule ufasaha nacho hatuna, tumebakia kukipopowa tu ndivyo sivyo, almuradi tumeandika au kutamka. Wahusika jaribuni kuhariri khabari zenu kabla yakutuwekea hapa, naamini miongoni mwetu tupo tunaokereka tunapogunduwa makosa ya kupuuzipuuzi kama hayo, khatma yake badala ya kujadili/kuchangia mada/hoja husika, unajikuta unaanza kwa ukosowaji na usahihishaji wa habari hiyo. Wahusika tafadhalini kuweni makini na kazi yenu msifanye almuradi tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...