Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa picha ya X-Ray, ya mmoja kati ya majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya Mount Meru, Joseph Anthony, mkazi wa Karoleni, baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema eneo la Soweto jijini Arusha. Imeelezwa kuwa hadi jana Juni 17, 2013, wakati makamu alipowatembelea majeruhi hao watu watatu waliliripotiwa kufariki dunia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa jijini Arusha waliokusanyika nje ya Hospitali ya Mount Meru jana, wakati Makamu alipokuwa na ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema jijini Arusha, ambapo jumla ya watu 70 walijeruhiwa na watatu walifariki dunia. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Selian, mkoani Arusha baada ya kudaiwa kushambuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Kata ya Makuyuni, Monduli. Awali Nasari alikaririwa akieleza kuwa anamaumivu ya mgongo baada ya kushambuliwa na vitu vigumu na vijana wa Kimasai. Kwa mujibu wa maelezo ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Kweka, anayemtibu Mbunge huyo, alimueleza Makamu wa Rais kuwa mbunge huyo, baada ya kupimwa na kupigwa picha za X-Ray, ameonekana kuwa hana tatizo lolote la kiafya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Geofrey, kuhusu jinsi mtoto, Aboubakar Adam, mkazi wa Sakina jijini Arusha, aliyelazwa katika Hospitali ya ARumeru baada ya kujeruhiwa na bomu wakati akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katika Uwanja wa Soweto kwenye Mkutano wa Chadema wiki iliyopita. Makamu wa Rais, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo, waliolazwa katika Hospitali za Arumeru, Selian na Mtakatifu Elizabeth, jana Juni 17, 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2013

    Sasa kama Nasari hana ugonjwa wowote kwa nini wamemlaza? Au siku hizi maamuzi ya either ulazwe au usilazwe ni ya mgonjwa/mzima?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2013

    A NORMAL X RAY OR MRI/CT SCAN DOES NOT RULE OUT PRESENCE OF AN ILLNESS, AND IN THIS CASE AN INJURY, HE MIGHT NOT HAVE FRACTURED A BONE, BUT HE HAS MOST LIKELY SPRAINED/STRAINED LIHAMENTS AND OR MUSCLES AS A RESULT OF THE CLAIMED ASSAULT.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2013

    Anon #1, ni maumivu tu, bakora za Kimasai mchezo! Anyway, nadhani anamaanisha hajavunjika kama ilivyodhaniwa Mwanzo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2013

    Mbona maelezo mazito sana ya mwenyekiti wa Chadema hujayaweka tukalinganisha?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2013

    Wewe anon hujaelewa kama Nassari alipigwa na kujeruhiwa na hali yake ni mbaya? mbona hueleweki?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2013

    Nassari suffering from MUNCHAUSEN SYNDROME.Lol

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2013

    Usipoteze muda kusoma hii ngonjera, hapo walikuwa wamasai katika moja ya ngoma zao za jadi. Kutandikana fimbo !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...