Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari wa saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni huki Darfur nchini Sudani wakati wakilinda amani,yakishushwa kwenye Ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,Jijini Dar es Salaam leo alasiri.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki duni Darfur wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipakia  moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia huko Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.

Miili ya Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki Dunia wakati wakiwa katika kazi ya kulinda amani kwenye Mji wa Darfur nchini Sudan,imewasili nchini leo majira ya alasili kwa kutumia ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.

Askari hao waliuwawa kwa shambulio la kushtukiza na kundi la waasi wakati wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda amani nchini Sudan.

Jeshi la JWTZ lilitoa taarifa likisema kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2013

    So sad, may allah rest their soul in eternal peace, I personally argue Tanzanians to be pattient at this difficult time .
    Respect to all soldiers in the country!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2013

    Natoa pole kwa famila za marehemu.
    Mungu apunzishe Roho zao mahali pema peponi.
    Amen

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2013

    R.I.P mashujaa wetu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2013

    Wakati umefika wanajeshi wetu tusipeleke bila ya kuwa na silaha za kujihami. Huwezi kulinda amani bila ya mlinzi mwenyewe kuwa na silaha ya kujihami.

    ReplyDelete
  5. Che GuevaraJuly 21, 2013

    RIP you all,inauma sana jamani!
    Serikali imesema kila familia inapata fidia ya shs milioni 113, fedha hizo ziwafikie wajane kwa ajili ya watoto na sio kwa mashemeji au mawifi tafadhali!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2013

    Hakika tutawakumbuka daima mashujaa wetu,poleni sana wafiwa,tupo nanyi ktk wakati huu mgumu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2013

    Tuhakikishe msiba huu hauna mko wa maadui wetu.(M23 na Kagame)Kama kuna mkono wa Kagame then TUMSHIKISHE ADABU kama tulivyo fanya kwa NDULI wa Uganda.When it came to milirary "We are the supper power in East Africa".
    POLE kwa WAFIWA wote
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...