Msimamizi wa Masoko na Biashara wa Tigo, Gaudens Mushi akimtazama mmoja ya washindi wa droo ya tano ya Promotion ya Miliki Biashara yako na Tigo, Furaha Hasani akipunga mkono kwa watu mara baada ya kukabidhiwa Bajaji yake katika eneo la Tandika Jijini Dar es Salaam.
Meneja Uzalishaji Tigo, Hussein Seif akimkabidhi funguo ya Bajaji mmoja ya washindi wa droo ya tano ya Promotion ya Miliki Biashara yako na Tigo, Bi Happines Ndeki Mkazi wa Kinondoni (Kushoto) mara baada ya kukabidhiwa Bajaji yake katika eneo la Tandika Jijini Dar es Salaam.
Bajaji kuimiliki si haba mwanawane!
ReplyDeleteBaada ya mshikemshike wa usafiri mbovu , kwa kuzunguka na mabasi hadi kituo cha mwisho na kupandia madirishani hatimaye wamefanikiwa nao kuingia Petrol Stesheni kujaza mafuta badala ya kugombaa na Makondakta na wapiga debe wa Mabasi!
Wenye nyumba msije kuona wamemiliki Bajaji mkawapandishia Kodi za Nyumba!
Sio nini wala nini hata wenye nyumba mnaeza kuingia kwenye Droo nanyi mkaibuka Washindi!