Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni Mjumbe wa Nec CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza  na mtandao huu jana jioni alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji kutobomoa nyumba na vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu bila kufikia muafaka kwa mazungumzo na wahusika.

Zoezi hilo la kubomoa eneo hilo ili kujengwa barabara ya mtaa lilianza tangu mwezi wa tano mwaka huu, ambapo wenye nyumba zizizopo eneo hilo baada ya mazungumzo na wasimamizi wa zoezi hilo na Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, walikubaliana na kuwekewa alama eneo linalotakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi huo.

Baada ya alama hizo ulifanyika ubomoaji na kuchimba barabara hiyo kana kwamba zoezi la ujenzi lilikuwa likianza muda mfupi tu baada ya ubomoaji, lakini cha kushangaza watu wao baada ya kubomoa waliondoka zao na kuacha eneo hilo likiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji na kusababisha eneo hilo kutopitika kwa wenye magari na waenda kwa miguu.

Aidha baada ya kumalizika kwa ubomoaji huo, wahusika wenye nyumba zao na fremu za maduka eneo hilo, walikaa kwa muda wa miezi miwili na walipohakikishiwa kuwa zoezi hilo limemalizika na hakuna ubomoaji utakaoongezeka, walianza kukarabati nyumba na fremu zao upya ili kuendelea na biashara.

Cha kushangaza ghfla watu hao walirejea tena jana na kuchora alama mpya kwa kutumia mkaa, na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo jambo lililowaacha hoi wananchi wa eneo hilo na wenye frem zao, kutokana na kutotolewa kwa taarifa wala watu hao kutokuwa na kiongozi hata mmoja wa Eneo hilo yaani Diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambao walitakiwa kuwepo ili kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.

Lakini cha kushangaza wakati wa zoezi hilo, hakuwepo Mwenyekiti wala Diwani, jambo lililowafanya wananchi kuhoji juu ya uhalali wa zoezi hilo.

Wakati wa zoezi hilo Asha Baraka, alimpigia simu Diwani, Abasi Tarimba, lakini naye alimjibu kuwa hajui lolote kama Diwani na kumtumia namba ya simu ya mtu mwingine ili azungumze naye, wakati yeye ndiye hasa alitakiwa kuwapo eneo hilo na kuwatetea wapiga kura wake.

Hata hivyo watu waliokuwapo eneo hilo walishangazwa na kitendo cha jamaa hao kuendelea kumoboa upande mmoja wa eneo hilo huku wakikwepa ukuta wa ghorofa lililopo eneo hilo ambalo ni jipya lililojengwa hivi karibuni kwa kukwepa gharama, wakati alama za awali zinaonyesha kuwa hata ukuta wa ghorofa hilo ulitakiwa kubomolewa.
 Katapila likiendelea kubomoa....

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Eti "Maisha ni Nyumba" huku Nyumba zinabomolewa nchi nzima. Big Resuts Now. Watanzania cha moto tunakiona.

    ReplyDelete
  2. Zinahitajika taarifa zaidi kuwezesha comments kamilifu

    ReplyDelete
  3. Tanzania hiyo bwana, ofisi nyingi za umma watendaji hawajui sheria. Nafikiri kila mtumishi wa wananchi ajue kwamba ATOE HAKI BILA KUOMBWA KWA MAANA NYINGINE ATOE HUDUMA BILA KUOMBWA HATA KAMA MHUDUMIWA ATAKUWA AMEJISAHAU.

    ReplyDelete
  4. Ina maana wa TZ wote mbumbumbu? Mtu anakurupuka kutoka anakotoka anavinja nyumba za watu tu?

    Huu ni wivu uliojengeka. Hawa wavunjaji nina uhakika hawana kitu, hawajui mali huwa zinatfutwaje.

    Wanakaa kuharibu mali za wengine bila hata huruma.

    Tz kazi mnayo

    ReplyDelete
  5. Mbona mie nimebomolewa ghorofa wakati nina vibali vyote huku boko mbona hapakuwa na kelele?

    ReplyDelete
  6. Naona hawakujui hao, ebu waonyeshe kazi wakujue.

    ReplyDelete
  7. epukeni kujenga maeneo ya barabarani bila kuacha nafasi ya kutosha kwani gari inaweza kuacha barabara ikaingia ndani/ chumbani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...