Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini zimeshauriwa kutumia Mkongo wa mawasiliano ili kuchochea shughuli za maendeleo ya kijamii na uchumi. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa aliawambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kuziunganisha nchi hizo na mkongo wa mawasliano. 
“Mkutano wetu leo umeshirikisha wajumbe kutoka nchi nane zikiwemo za Kenya, Rwanda, Angola, Sudan, Uganda na Burundi,” lengo likiwa ni kupanua wigo wa matumizi ya mawasiliano kupitia mkongo huo. 
Alisema Tanzania tayari inapata mawasiliano kupitia mkongo wa taifa na ile ya kimataifa inayopita chini ya bahari ikiwemo ya Ezecom na Celcom kwa mawasiliano ya kimataifa. Alifafanua kwamba mafanikio hayo yamewezesha pia nchi kama Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi na Uganda kunganishwa na mkongo wa Tanzania. 
Pia Tanzania ipo mbioni kuziunganisha nchi nyingine kama Sudan Kusini na Msumbiji kupata huduma hiyo hiyo muhimu kimaendeleo. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura alisema mkongo umesaidia nchi kuhama kutoka katika mfumo wa Analojia kwenda katika matangazo ya Dijitali. 
“Tunatarajia pia nchi nzima itapata matangazo yake kwa mfumo huu wa dijitali baada ya kuzima analojia katika maeneo yaliyobaki,”alisema. 
Alisisitiza kwamba matumizi ya mkongo wa mawasiliano ni rahisi na huduma hiyo kupatikana kwa bei nafuu. Mkongo ni muhimili wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo kwa sasa TTLC imeshinda tenda ya kutoa huduma ya internet kwa serikali ya Tanzania na Rwanda kwa miaka 10. Pia nchi imeweza kupata wateja waliounganishwa na mkongo wa mawasiliano wa Tanzania. 
Waziri wa Sayansi na Mawasiliano wa Sudan, Dkt. EIsa Bashari Mohmed Hamid alisema mkutano huo umetoa changamoto kubwa kwa nchi yake kujiunga na mkongo wa Tanzania. “Tuna mawasiliano ya karibu na nchi ya Tanzania katika kufanikisha jambo hili,” na hii ni huduma muhimu kwa maendeleo kwa vile ni rahisi na inapatikana kwa bei ya chini.
 Alisisitiza kuwa mawasiliano yakiwa ya uhakika husaidia wananchi kupata maendeleo. Mkutano huo ulishirikisha nchi nane na uliandaliwa na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Waziri wa Mawasliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa matumizi ya Mkongo wa Mawasiliano katika kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, kushoto ni Waziri wa Sayansi na Mawasiliano wa Sudan, Dkt. Eisa Bashari Mohmed Hamid wa Sudan na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA, Profesa John Nkoma, mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi nane.
Waziri wa Mawasliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akichangia mada  wakati wa mkutano wa matumizi ya Mkongo wa Mawasiliano katika kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini,wapili kushoto ni Waziri wa Sayansi na Mawasiliano wa Sudan, Dkt. Eisa Bashari Mohmed Hamid wa Sudan, Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano nchini (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA, Profesa John Nkoma, mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi nane.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mm huwa nakeleka sn moyoni kukimbilia kuwapa watu wengine faida kabla ya ww mwenyewe hujakitumia vizuri hiko kitu,hakikisha NCHI yako ya TANZANIA imetosheka kwanza ndio uhamie kwa wengine,coz haiwezekani hata sikumoja chakula kidogo nyumbani kwako kisha ukakigawe kwa majilani zako BORA nionekane MCHOYO kuliko KUIUWA FAMILIA YANGU,kwanza nyumbani na wala sivinginevyo,balozi wa MAREKANI ametwambia tuzingatie neno TANZANIA KWANZA,lakini wapi? Kwa viongozi wetu wao wako kinyume na hilo neno,NNJE KWANZA Tanzania baadae yaani ajabu sn

    ReplyDelete
  2. Hongera Waziri na wafanyakazi wote wa Wizara ya Mawasiliano. Nani amesema kwa kuziunganisha nchi nyingine kwenye mkongo huu Watanzania wanakosa kitu. Mambo ya maendeleo yanakwenda sambamba ndani ya Nyumba na nje. He kalagabaho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...