Mbunge Amina Mwidau, akihutubia wanannchi wa Wilaya ya Pangani katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoa wa Tanga.
Mbunge Amina Mwidau, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa Timu ya soka ya wanawake ya Spin Sister, Habiba Hamisi. Timu hiyo ipo Marizala Pongwe jijini Tanga.
 ========  ======== =======

Mwidau ataka kasi ya maendeleo Tanga
Na Mwandishi Wetu, Tanga.

MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kubadilika kwa kuwa na ari ya kujiletea maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa mjini hapa alipokuwa akizungumza na vionozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (Tanga Press Club).
Alisema kuwa ili maendeleo ya haraka yaweze kupatikana katika mkoa huo ni lazima jamii kubadili kwa kuwa na mawazo chanya.

“Maendeleo ni jambo muhimu sana na katika hili ni lazima tushirikiane kwa dhati. Binafsi ninapenda kupongeza juhudi za chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya katika kutangaza mkoa wetu.

“Nilikuwa nasoma na sasa kila wakati tutakuwa pamoja na wanahabari pamoja na wananchi wa mkoa wetu ili kuweza kuungana kwa pamoja katika juhudi za maendeleo za mkoa,” alisema Mwidau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mdau wa wanawakeOctober 30, 2013

    KATI YA MANENO ALIYOONGEA ANGEPATA SUMMARY YA UJUMBE WA JEZI BADALA YA KUANDIKA JINA LAKE>IT DOESN't make sense. waandishi wa tanga mshaurini mhe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...