Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana  akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani Tunduru mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.Kinana na Ujumbe wake kesho ataelekea Wilayani Namtumbo kuendelea kukagua miradi ya mbalimbali ya Wananchi na chama kwa ujumla.
Sehemu ya wakazi wa Tunduru mjini  wakishangilia  jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Maeleoz yakitolewa namna ya Korosho zinavyochambuliwa mara baada ya kubanguliwa na mashine ya kisasa,ampapo zao hilo la biashara linalotegemewa na wakulima wa Wilaya ya Tunduru wamekuwa wakilalamikia suala la bei kuwa ndogo inayopangwa na Wanunuzi hali inayowapelekea Wakulima wa zao hilo kukata tamaa na maisha yao kuendelea kuwa duni siku hadi siku.
Msimamizi wa Kiwanda cha Korosho,Korosho Africa Ltd akifafanua namna ya Korosho zinavyobanguliwa kwa kutumia mashine za kisasa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Kinana na Ujumbe wake wanamalizia ziara yao leo ndani ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kesho kuwasili ndani ya Wilaya ya Namtumbo kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya chama na wananchi sambamba na miradi.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,akizungumza na akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa mapema leo mchana walipokwenda kutembelea kiwandani hapo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na akina mama wanaofanya kazii ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa,ambao baadhi ya akina mama hao walilamika suala la ujira wanaolipwa kuwa ni mdogo na haukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Uchambuzi wa Korosho ukiendelea.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA NA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani hawa kina mama wanahitaji teknolojia mpaka Leo bardo wanatumia mikono! Sasa huyo waziri anasemaje au ni kujionyesha tuu aka kuuza sura

    ReplyDelete
  2. Bila shaka mdau hapo juu, a.k.a kuuza sura, si wenyewe tunawajua viongozi wa bongo bra bra tu za kuhuza sura na kupoteza muda, watu siku hizi wameamka katika bara hili la giza, kwa hiyo tusidanganyane,tuende na wakati sio kuuza sura tu,

    ReplyDelete
  3. Sido mko wapi? Viwanda kama hivi vinahitaji machine za kurahisishia kazi. Kun mashine kama za kubangulia karanga mkiziangalia kwa makini mnaweza kutengeneza za kubangulia korosho vile vile. Itasaidia kuongeza ufanisi na wakulima watazalisha zaidi kama watapata soko bora kwa bidhaa zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...