Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihitimisha
ziara yake mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani Tunduru mkoani Rukwa na
kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.Kinana na Ujumbe wake kesho
ataelekea Wilayani Namtumbo kuendelea kukagua miradi ya mbalimbali ya
Wananchi na chama kwa ujumla.
Sehemu ya wakazi wa Tunduru mjini wakishangilia jambo wakati Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake
mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na
kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Maeleoz yakitolewa namna ya Korosho zinavyochambuliwa mara baada ya kubanguliwa na mashine ya kisasa,ampapo zao hilo la biashara linalotegemewa na wakulima wa Wilaya ya Tunduru wamekuwa wakilalamikia suala la bei kuwa ndogo inayopangwa na Wanunuzi hali inayowapelekea Wakulima wa zao hilo kukata tamaa na maisha yao kuendelea kuwa duni siku hadi siku.
Msimamizi wa Kiwanda cha Korosho,Korosho Africa Ltd akifafanua namna ya Korosho zinavyobanguliwa kwa kutumia mashine za kisasa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Kinana na
Ujumbe wake wanamalizia ziara yao leo ndani ya Wilaya ya Tunduru mkoani
Ruvuma na kesho kuwasili ndani ya Wilaya ya Namtumbo kukagua shughuli
mbalimbali za maendeleo ya chama na wananchi sambamba na miradi.


Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,akizungumza
na akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha
Korosho Africa mapema leo mchana walipokwenda kutembelea kiwandani hapo
na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na akina mama
wanaofanya kazii ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho
Africa,ambao baadhi ya akina mama hao walilamika suala la ujira
wanaolipwa kuwa ni mdogo na haukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Jamani hawa kina mama wanahitaji teknolojia mpaka Leo bardo wanatumia mikono! Sasa huyo waziri anasemaje au ni kujionyesha tuu aka kuuza sura
ReplyDeleteBila shaka mdau hapo juu, a.k.a kuuza sura, si wenyewe tunawajua viongozi wa bongo bra bra tu za kuhuza sura na kupoteza muda, watu siku hizi wameamka katika bara hili la giza, kwa hiyo tusidanganyane,tuende na wakati sio kuuza sura tu,
ReplyDeleteSido mko wapi? Viwanda kama hivi vinahitaji machine za kurahisishia kazi. Kun mashine kama za kubangulia karanga mkiziangalia kwa makini mnaweza kutengeneza za kubangulia korosho vile vile. Itasaidia kuongeza ufanisi na wakulima watazalisha zaidi kama watapata soko bora kwa bidhaa zao.
ReplyDelete