Mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA, Georgina Lema
Moja ya sababu zilizotusukuma kujadili masuala kuhusu FAMILIA ZA KAMBO ni takwimu zilizopo hivi sasa kuhusu familia hizi.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.blendedandbonded.com, hapa Marekani
• 41% ya ndoa za kwanza huishia kwenye talaka
• 60% ya ndoa za pili huishia kwenye talaka
• 73% ya ndoa za tatu huishia kwenye talaka
• 45% ya wanawake na 50% ya wanaume wataoa tena ndani ya miaka mitano ijayo
• 50% ya ndoa za marudio huhusisha watoto wa mahusiano yaliyopita walio chini ya miaka 18
•Ndoa 2100 huanzishwa kila siku nchini Marekani
• 42% ya watu wazima wana uhusiano wa kambo. Hii inajumuisha mzazi wa kambo / mtoto wa kambo ama ndugu wa kambo
Kwa idadi ya Marekani, takwimu hizi zinamaanisha kuwa familia za kufikia zinahusisha watu wazima wapatao milioni 95.5
•Kuna baba wa kambo milioni 16.5
•Kuna Mama wa kambo milioni 14.
•Wataalamu wa mahusiano wanasema kuwa ndoa za kufikia ndio zitakuwa ndoa zenye umaarufu na nyingi zaidi nchini Marekani na kuwa, kutokana na kukosekana kwa taarifa sahihi kuhusu familia za kufikia, familia hizi mara nyingi zimejikuta kwenye migogoro na mafarakano.
Nasi tuko hapa kujaribu kuepusha hilo kwa kushirikiana nanyi katika kile tunachoweza kuelimisha kudumisha ndoa hizo.
Ungana nasi katika sehemu hii ya mwisho ya MADA hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Michuzi, kuna siku nilikuandika wabonyeze wazee wakazi wafanya ambush kwenye maeneo yenye maukuta marefu zaidi ya prison sijui umefanya hiyo kazi? Tumeona wenyewe wachina waliokamatwa juzi na meno ya tembo,sasa kaka kule kwenye magodauni kurasini ndiko kwenyewe!!! Take it from me. Usiitoe hii humu ndani. Pleaseplease Michuzi hawa wawekezaji wanatumaliza jamani. Nina uhaikika naninachosema. Mpaka silaha zipo huko.

    ReplyDelete
  2. Nawapongeza kwa kipindi kizuri.

    Mmetoa takwimu nzuri, lakini hamjatoa sababu za wanandoa kuachana.

    Pili naomba mpunguze kusema "Am" inapunguza mtiririko au inaonekana kama hamna uhakika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...