Kwa ukakamavu kijana wa CCM akimvisha kitambaa Mh.Mwigulu nchemba mara baada ya kuwasili kwenye kambi ya mafunzo ya vijana wa CCM-Namtumbo
CCM oyeeeeee!!!Naibu katibu mkuu akisalimiana na vijana wa CCM wakati akiingia eneo la tukio.
Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi Mh.Mwigulu Lameck Nchemba leo Tar.31/10/2013 amefunga rasmi mafunzo ya vijana wa CCM (UVCCM) yaliyofanyika kwa muda wa wiki mbili hapa Ruvuma Wilaya ya Namtumbo.
Mafunzo haya yaliyojumuisha wilaya zote za Ruvuma kwa vijana wa CCM yalilenga kuwajengea uwezo vijana wa kutambua Umuhimu wao katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ndani ya nchi yao,siasa za nchi na mwenendo wake,Uelewa kuhusu namna ya kufanya maamuzi sahihi katika umri wake huu wa ujana,pia kuwaandaa kifikra na kimaadili kwaajili ya kuijenga na kuimarisha CCM pamoja na jumuia zake hasa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi.
NIZI KAMBI ZA MGAMBO WA CCM KWANINI ZINAONEKANA NI NEEMA LAKINI ZA VYAMA VINGINE VINAONEKANA NI LAANA?
ReplyDelete