ya pili mfulizo ambapo wafanyabiashara wakiwa wamekutana katika Ukumbi M M hotel kuunda Umoja wao ili kupinga ongezeko la kodi mbalimbali pamoja na Mpango wa Mashine za TRA kwa Wafanyabiashara wadogo.
======= ======= =======
Na Abdulaziz Video
Wakazi wa Manispaa ya Lindi Wameendelea kukosa huduma ya kununua
bidhaa za madukani ikiwemo vyakula kwa siku ya pili mfululizo
kufuatia mgomo ulioitishwa na wafanyabiashara kutokana na kodi kubwa
inayotozwa na mamlaka ya mapato ikiwemo kodi ya huduma inayotozwa na
halmashauri ya manispaa ya Lindi
Kufuatia mgomo huo wafanyabiashara hao walikutana katika ukumbi wa
Double M hotel na kuazimia kuendelea na mgomo hadi wenzao
waliofikishwa mahakamani kwa ajili ya kodi ya Huduma kuachiliwa
Habari zaidi tutawaletea hapo baadae..
Wakazi wa Manispaa ya Lindi Wameendelea kukosa huduma ya kununua
bidhaa za madukani ikiwemo vyakula kwa siku ya pili mfululizo
kufuatia mgomo ulioitishwa na wafanyabiashara kutokana na kodi kubwa
inayotozwa na mamlaka ya mapato ikiwemo kodi ya huduma inayotozwa na
halmashauri ya manispaa ya Lindi
Kufuatia mgomo huo wafanyabiashara hao walikutana katika ukumbi wa
Double M hotel na kuazimia kuendelea na mgomo hadi wenzao
waliofikishwa mahakamani kwa ajili ya kodi ya Huduma kuachiliwa
Habari zaidi tutawaletea hapo baadae..


Msishindane nao,wapeni siku tatu tu, watarudi wenyewe. Kwanini kila mtu anataka kubembelezwa siku hizi? Kumbukeni hii nchi ni yetu sote Watanzania na hakuna mwenye haki kumzidi mwenzake.
ReplyDeleteChondechonde serikali mkifanya mchezo kwenye kukusanya mapato tutajuta,,ikumbukwe ya kwamba muungano wa EAST AFRICA unaenda kufa kwa upande wetu so msifanye mchezo kwenye eneo hilo,hao wanaogoma vitu vyote vichukuliwe viwe chini ya serikali ndio itakua mwalubaini wao na kwa wengine pia,jamani ndugu zangu watanzania mm huku nilipo UINGEREZA kama utaenda kinyume na matakwa ya serikali basi maisha yako yatakua na uzito wa sufi,, ndio maana wenzetu wameendelea na kupiga hatua kubwa sn mbele coz hawana masihara kabisa na hayo mambo ya UKUSANYAJI WA MAPATO,,amkeni kwenye usingizi na muwe wepesi wa kulipa hizo kodi kwa faida ya NCHI YAKO,naitwa mdudu kakakuona,
ReplyDeleteManispaa ikipata kodi ikumbuke kuweka lami sehemu hizo pia
ReplyDeleteSisi wafanyakazi wa Serikali huwa tunakatwa kodi kubwa sana (asilimia thelathini ya mshahara wako) lakini wafanyabiashara wao wamepewa mashine hawataki kuitumia wanaogopa kodi.
ReplyDeleteKama alivyosema mdau hapo juu mukifanya dharau basi tutaangukia pua?
TRA jee munajua kwamba baadhi ya wafanya biashara wakubwa hapo uhindini huwa wanaficha hizo EFD zenu na ukienda kununua bidhaa wanakwambia eti njoo kesho maana leo mashine imeharibika?
FUATILIENI MUTAWAONA.
wee unaye ongea wa pili, huna wala hujui biashara, makampuni ya kuchimba madini yanapakua na hawalipi chochote, mzawa na kabiashara chake unataka ukamue, embu nenda ukafikirie mara mbili juu ya ulichokiandika, wafanyabiashara hajakataa kulipa kodi,wanapinga uongezekaji wa kodi, na installation ya machine za TRA
ReplyDeletemdau wa maoni wa pili ni sawa unayosema .LAKINI juwa kuwa hapa UIENGEREZA (UK) the system is fair and transparent sio kama huko BONGO.
ReplyDeleteKwani nani hajuwi kuwa kuna matajiri wakubwa tu hawalipi kodi ? Munawabana hao masikini tu. Kama anavyosema rafiki yangu 'its always poor who suffer.
Pia wafanya biashara kule zanzibar munawalipisha kodi mara mbili yaani ZRB na TRA ndani ya nchi moja ya TANZANIA !.
Hivi sasa hapa UK Wales watakuwa na tax system yao bila ya kuingiliwa na westminster nategemea kuwa umesikia camera man akisema hivi karibuni.
Kusanyeni kodi na weka siasa pembeni na hakikisheni kodi yetu inatumika vizuri na si vinginevyo. Jamani kodi ndio kila katika maendeleo; mdau anasema makampuni makubwa yanakwepa kodi nae ametulia kimya na anataka wengine nao wakwepe sasa maendeleo yatakuja kwa miujiza ipi!
ReplyDeleteNimependa HAKIMU'S OFFICE!!!
ReplyDelete