Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini , Afande Pius Nyambacha ( aliyesimama) akisoma maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa ,kufungua kikao cha kazi cha Makamanda wa Mikoa na makao makuu wa Jeshi hilo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Edema ya Mjini hapa ( wapili kutoka kulia) ni Naibu Kamishina Jenereli wa Jeshi hilo nchini, Lidwino Simon Mgumba.
Baadhi ya Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimsililiza mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa ( hayupo pichani), leo wakati wa kufungua kikao cha kazi cha Maofisa wa ngazi za juu na Makamanda wa Mikoa pamoja na watumishi raia katika ukumbi wa Hoteli ya Edema, ya Mjini Morogoro
Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akifungua kikao cha kazi cha Maofisa wa ngazi za juu na Makamanda wa Mikoa pamoja na watumishi raia katika ukumbi wa Hoteli ya Edema, ya Mjini Morogoro
Juu na chini ni Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Lilian Mapfa ( kati kati walioketi) katika picha ya pamoja na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji , Pius Nyambacha ( wanne kushoto) na ( watatu kutoka kulia ) ni Naibu Kamishina wa Jeshi hilo, Lidwino Simon Mgumba, pamoja na wageni waalikwa kutoka Idara ya Uhamiaji, Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro sambamba na Makamanda wa Mikoa wa Jeshi hilo , mara baada ya Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, baada ya kufungua kikao cha kazi Novemba 11, mwaka huu ukumbi wa Hoteli ya Edema, ya Mjini Morogoro. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro.


Laptop zinatumika hadi kwenye Majeshi ya Zimamoto?
ReplyDeleteKwa kasi hii ya Dijitali kwa akina Sajenti Marwa kuweza ku 'browse' nchini mnapo haribu mtatafutwa kwa mtandao ni muda wa ninyi Wahalifu mkalime!!!!
Uhalifu sasa basi!
Mnapobisha mkisema Miaka zaidi ya 50 ya Uhuru Tanzania hakuna maendeleo nakataa,,, Polisi iliyokuwa inajulikana kwa matumizi makubwa ya makabrasha na makaratasi sasa inatumia Laptop na internet!!
ReplyDeleteWengi hubisha kwa nongwa na bila vigezo!!!
ReplyDeleteSasa Polisi wanatumia Laptop?
Mkisema Jakaya Kikwete hajaleta Maendeleo Tanzania mtakuwa wanafiki kama ''Coalition of the willing'' katika Afrika ya Mashariki!
Arooo Afande Kyaruzi !!!
ReplyDeleteRogi in kwenye inteneti haraka, ngoja niri tafute Riharifu katika FESIBUKU nikiri kosa humo nitarukia kwenye ISNTAGRAMU na kama rikini toroka NITA SIKANI picha yake na KUIEDITI na hapo ni razima tutari aresiti tu KIDIJITALI!!!
Ohhh!
ReplyDeleteNetiweki bado ipo chini, uripo kuja kuripoti hapa Polisi Positi nirianza kuritafuta rifaili rako online.
Rakini nitajitahidi kuripata Mutandaoni Fairi rako Rabda uniongezee Vocha !!!
Laptop ya mkufunzi au mtoa mada. Naona makanda wote wana kalamu na notepad na maji madogo ya kilimanjaro. Polisi bado hawajawezeshwa vya kutosha kupata vifaa vya kisasa kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu. Hata barabarani unakuta wako patrol hawana redio. Polisi wote wanatakiwa wapewe redio call....
ReplyDeleteKuna chama kimoja cha siasa chenye kudai kuwa tangu uhuru Tanzania hakuna hata tone la maendeleo; yaani, hakuna maendeleo yeyote.
ReplyDeleteNa mbumbumbu wanakisikiliza bila kujibu mapigo kwa kuwa kiongozi wake kasema hivyo.
Je kuwa na vyama vingi vya siasa sio maendeleo (political development)?
Shame on you, chama hicho!
Usiminye, Michuzi!