Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela.
Hapa Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji akiwa amemuweka begani na Kushuka nae chini Mara baada ya kufanikiwa Kumshika vizuri kwaajili ya kumteremsha chini bila kupata madhara
 Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Hassan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kushushwa juu ya Mnara wa Simu na Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji muda mfupi uliopita Ubungo jijini Dar.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Ni njia ya aina yake ya kuita Press Conference lakini ni hatari. Na kama angejirusha na kupoteza maisha sijui tungesema ni ajali za mwaka mpya?

    Sesophy

    ReplyDelete
  2. We have to expect this and many others to come,trying to deliver the message to those who still in a deep sleep, those who put cotton tags in their ears,those who close their eyes about what is going on in the society.

    ReplyDelete
  3. Hassan amefanya ubunifu hapa,

    Suala la Msingi Hassan angesema 'nahitaji mkono wende kinywani' badala ya Madai ya kuonana na Raisi Kikwete wakati licha ya kubambikiwa Kesi na Polisi tayari umeshatumikia kifungo cha miaka 6 Jela na sasa upo huru!

    ReplyDelete
  4. Wewe Hasasan upo Huru Uraiani emshamaliza Kifungo hadi unapata muda wa kupanda juu ya Mnara wa simu, huoni huo ni uhuru tosha?

    Nenda kafanye kazi upate fedha za kuendesha maisha yako kwa kuwa Madai hayatakusaidia chochote licha ya kuwa ulionewa na Polisi kwa vile tayari umeshafungwa miaka 6 na sasa umeshatoka!

    ReplyDelete
  5. Haya ni matokeo ya ukosekenaji wa haki. Polisi hawana checks and balances, kesi ya polisi inachunguzwa na polisi. Hakuna uwazi wala clear reporting systems kwa wananchi wa kawaida na hii ni mianya ya rusha. Hassan angejua wapi apeleke malalamiko yake ambapo angesikilizwa na yangechukuliwa hatua asingetaka aonane na Rais wa Jamhuri. Nchi hii ina mianya ya rushwa kibao na imewekwa makusudi uwanufaisha watu fulani.

    ReplyDelete
  6. Ohhh huyo Hassan ni kijana?

    Mtu anaonekana mtu mzima kabisa na mapengo kibao mdomoni meno hana au ndio kipigo alichopata cha Polisi hadi Lupango?

    Au ndio amezeeka kwa shida za Jela na msoto wa Maisha?

    ReplyDelete
  7. Ahhh wapi Hassan sio kijana!

    Kama ni uzee labda amezeeka kwa shida na changamoto za kimaisha, kama anavyodai ameonewa kwa kubambikiwa Kesi na Polisi.

    Uso wake ulivyo kakamaa na mapengo bado yeye tu ni kijana?

    ReplyDelete
  8. Ni kweli mdau hapo juu TZ mianya ya rushwa ni mingi sana na wakati mwingi ukosefu wa taarifa sahihi unatumika kuombea rushwa.
    1. kwenye ajira je ajira zote zinatangazwa kwa wakati na sifa na malipo kuwekwa wazi? siku hizi waajiri wengi wanadai rushwa ya mishahara ya miezi kadhaa au ngono or all of the above wanapoajiri vijana
    2. TRA haya ya nenda rudi kama sio rushwa ninini?
    3 Tanesco - unabambikiwa lideni usipolipa rushwa wanakukatia umeme.
    4. Elimu ya juu ndio usiseme - mitihani inasahihishwa na waalimu na kauli yao ni ya mwisho hakuna 'board of examinations' ambayo iko neutral to control the results - matokeo yake wasomi feki wanajaa mitaani
    5.Ukiishi nje unapokanyaga tu bongo kila unapokwenda wakijua umetoka nje unadaiwa rushwa
    6. Michuzi natoa hoja anzisha makala mwaka huu wa 2014 ya kupambana na rushwa, wahusika wajibu malalamiko ya wanajamii

    ReplyDelete
  9. Ndg. Hassan sio mzee inaonyesh ni ugumu wa maisha tu ndio tatizo huku mwenyewe akishindwa kuchanganua njia sahihi ya kuyafikia malengo ya Kimaisha!

    Ndio kama tunavyoona anafungwa Jela miaka 6 anatoka badala ya kupanga mikakati sahihi ya kujikwamua na changamoto za Kimaisha anapanda juu ya nguzo za mawasilaiano!!!

    Je, sasa Madai yako ukifikishwa kwa Mkuu itakusaidia nini wakati unatakiwa utafute mwenyewe njia zako kujinasua?

    ReplyDelete
  10. Huyu bwana Hassan wala si mzee kivile tatizo inaonyesha ana kasi sana ya kimaisha na matokeo yake anafikia kubambikiziwa ma-Kesi kama navyodai!

    ReplyDelete
  11. Hassan ni kiwakilisho cha Watanzania wengi kuhusu njia mbadala za kukabiliana na kasi ya maisha.

    Sasa ndugu yangu wewe kuonana na Kiongozi ndio itakuwa suluhisho la maisha?

    Are you serious?

    Be creative!

    ReplyDelete
  12. Hassan ni kiwakilisho cha Watanzania wengi kuhusu njia mbadala za kukabiliana na kasi ya maisha.

    Sasa ndugu yangu wewe kuonana na Kiongozi ndio itakuwa suluhisho la maisha?

    Are you serious?

    Be creative!

    ReplyDelete
  13. Hiyo kampuni ya simu ishtakiwe kwa kuhatarisha usalama wa raia, mnara wao ulipaswa kuwa umezungukwa na seng'enge, tena ikibidi ya umeme!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...